Posts

NEW YEAR RESOLUTION DON'T CHANGE YOUR CONFESSION

Image
HamasikaLeo Haujazeeka sana kiasi cha kughahiri malengo yako au kushindwa kuweka malengo mapya. Mambo mengine umekuwa  ukiyapanga na kupangua na kupanga kila mwaka bila mafanikio. Umekutana watu wanaojiita wahamasishaji kama huyu anayeandika na wamekufanya ujione kama hujawahi fanikiwa na kujisikia umechelewa na kukata tamaa. Ukipiga mahesabu ya mwaka 2016 hauoni fanikio la  kukufanya ufarijike na huenda ulipanga vizuri sana. Kuna ugonjwa fulani  wa mtu  kupanga kitu na unapofika muda wa utekelezaji hatekelezi mpaka muda unapita  na kupanga tena na tena, basi unakuwa  mchezo wa kupanga. Unajisikia ukakasi sana pale mwaka unapoisha hujafikia malengo yako au umefikia kwa kiwango hafifu. Wengi huwa tunabadili misimamo na kauli zetu tunapokutana na hali ya kutofikia malengo. Unaweza tumia mbinu hizo zinazoitwa mbinu za mafanikio na husionje hata harufu ya mafanikio na kuishia  kushawishika kukubaliana na hali halisi ya ugumu wa maisha. Takwim...

RAMANI YA KUTIMIA KWA MAONO YA MAFANIKIO

Image
HamasikaLeo Maono ya mafanikio ni zaidi ya kuongezeka kiuchumi, kuwa na cheo na kuwa na shahada. Kupanga juu  ya mafanikio kunahusisha nyanja zote za maisha. Kama ilivyo kwa ramani, unatakiwa kutambua mambo yafuatayo;- Mwanzo wa safari Mwisho wa safari Usafiri Mkoba wa kusafiria (Hazina  ya safari) Mwelekeo/Njia na kiongoza njia MWANZO WA SAFARI. ( Wewe ni nani kwa sasa) Ramani  ina  mahali pa kuanzia. Mahali pako  pa kuanzia ni kujibu swali hili kuwa wewe ni nani  kwa wakati huu?. Jibu lako litakuelezea hali  yako ya sasa kwamba ni mtu  wa aina  gani; ni wanafunzi, mfanyakazi, mfanyabiashara au mjasiriamali. Kupata muonekano zaidi wa mwanzo wa safari yako ni unatakiwa kuangalia kwa karibu imani yako, thamani yako na misimamo yako mbali na hali yako ya kiuchumi, kitaaluma na kijamii. Vile utavyojiona huwa ni tofauti na vile ulivyo. " Naitwa Peter, 19, ni mhitimu wa high school" Maneno ya Peter yanatuelezea juu ya ha...

NAMNA YA KUKABILIANA NA MAWAZO YATOKANAYO NA HOFU.

Image
HamasikaLeo Habari za uzima ndugu msomaji wangu. Bado tuna endelea na harakati zetu za kujifunza namna ya kutumia uwezo wetu wote tulionao kufanya mambo duniani. Leo tujikite kwenye swala zima la  mawazo na hofu katika mchakamchaka wa kufukuzana na maendeleo ya mtu  kuanzia kwenye mawazo ya kila siku. Ni kanuni ya maisha ya kila binadamu kuwaza, shida inakuja pale mawazo yako yanapotawaliwa na hofu, na wakati mwingine kushindwa kutofautisha wazo linalotokana na hofu au Lisilo la hofu. Wengi tunaamua kuishi tu maisha yaendelee. Kama muda wote unawaza kiasi gani maisha yalivyo magumu kwako, muda wote utahisi kuwa wewe mi maskini kuliko wote. Hofu ya maisha na kujiona hujafanikiwa hakupelekei mambo mazuri kukujia. Kama unataka kubadilisha maisha yako, badili namna unavyofikiri....na vile unavyosema kwa sauti mbele ya watu. Je, unayowaza na kusema yanatokana na nini? Ni muhimu kufahamu kuwa haijarishi ni kiasi gani tatizo lako ni kubwa, ni kwa kiwango gani tatizo lim...

KANUNI 16 ZA KUISHI MAISHA YAKO.

Image
rethink relive Habari yako ndugu msomaji wangu, wa mfululizo wa machapisho yanayogusa maisha yetu moja kwa moja hususani uwezo tulionao wanadamu wa kutufanya tuishi. Maisha yanakila kitu tunachotaka ila maisha hayatupi tunachotaka bali hutupa tunachotafuta kwa kuanza na kunia kupata. Leo tuangazie kona ya kuishi maisha yetu halisi, Tambua unawajibu wa kuishi maisha yako sio maisha ya mtu Fulani mashuhuri au mzazi wako. Maisha yetu yanaweza kutiwa hamasa na mtu ila sio kigezo cha kuishi kama yeye binafsi naita huo ni uvivu wa kufikiri. Hizi ni kanuni kumi sita za kuishi maisha yako. Penda kupenda . Upendo ni hali  ya asili ila  inataka utayari wa mtu husika, katika upendo mambo mengi yanafanikiwa, upendo ni dawa sio ya homa bali ya maisha kwa ujumla. Ndio maana vitabu vya kiimani imesisitiza sana, na kikristo upendo ni Mungu, yani Mungu ndio pendo. Ukitaka kuishi maisha yako kuna upendo unatakiwa kuwa nao, ni ule unaotokana na Mungu yani unaweza  mpenda  m...

LATE MWALIMU NYERERE J.K LEGACY

Image
rethink relive Mwalimu ni kiungo kikubwa cha maendeleo kama akijitambua na kutambulika na jamii husika yenye uhitaji huo. Mwalimu Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 April 13 kijijini Butongo, mzanaki huyu hakuwa mzanaki ilipofika wakati wa kupigania Uhuru na ukombozi. Hi heshima kubwa kushirikishana mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika kupigania Uhuru wa taifa na bara lote la  Africa. Kiongozi ambaye maamuzi yake na hoja zake zilileta matokeo chanya kwa  taifa. Alisaidia kuundwa kwa TANU Mwaka 1954 kuwa chama cha kisiasa jambo lililo mchukiza gavana wa uingereza Sir.Richard Gordon Turnbull. Alifanya maamuzi magumu ya kuacha kazi ya ualimu  akiwa Mwalimu Pugu sekondari kama sehemu ya masharti aliyopewa na gavana kuwa achague moja kati ya siasa  au kazi. Alishikiria maslahi ya wengi kuliko yake... "Niliogopa. Nikamuuliza Julius ikiwa ninachokisikia ni kweli, alipojibu ndio nikaogopa zaidi. Nikamwambia anachokifanya ni kibaya, Mungu amempa kazi unataka kuiha...

DO IT BEFORE 30's

Image
Have you ever heard of that term "forever young". Living like young person while you are old, is a dream of every person. In fact you can't stay young all of your life but you can challenge a chronological aging by maintaining a young like life. Everything starts from your mind. People says that thoughts can't be diagnosed, which is not right. Thoughts can be known right from your living. What you think can habitually manifested through what you eat, wear, speak, watch, spend time with and so many others. Here down are things to do when you feel like aged and you have made a decision of staying young until a gate way to unknown world comes. IMPORTANT THINGS TO DO BEFORE YOU TURN 30's Congratulation for being such aged. You’re still young, but you’re starting to move into fully-mature adulthood. So how exactly should you change you life for the better? There are things to do before you turn 30. It will be better to begin at 20's specifically 24 for...

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

Image
Habari ya uzima ndugu msomaji wangu, natumaini u mzima wa afya. Nimekuwa natamani kuandika kila mara, ningelikuwa mtoto mdogo ningechora kwenye mchanga. Leo tuangazie kuhusu kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa. Maneno haya yanabebana kimantiki licha  ya kutofautiana katika matumizi. Kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa ni kati ya mambo yanayojitokeza kwenye maisha ya wengi wetu. KUJIKATAA;- Siku yako ya kwanza kufunguka ufahamu na kuelewa namna  ulimwengu ulivyo ndio ulichukua hatua  ya aidha kujikubali au kujikataa. Mungu ni fundi  wa ajabu alitaka maisha yetu yote tuishi tukihamasishana kwa vile tulivyotofauti tofauti. Amempa mtu  mmoja hekima mwingine busara sio kwamba mwenye hekima ajidharau kwa kukosa busara, ila  waishi ulimwenguni wakijifunza na kubadilishana ujuzi. Mawazo ulioweka juu  yako kuhusu hadhi uliyonayo, elimu,pesa, mwonekano na vingine, ndio yanapelekea ujenge mtazamo wa kujikataa. Inashangaza sana kuona akina Dada wana...

KUWA WEWE

Image
rethink  KUWA WEWE umewahi jiuliza unapenda kuwa nani kwenye maisha yako? au umewahi kuulizwa unapenda kuwa nani kwenye maisha yako?, wengi hutoa majibu ya ajira wanazopenda na wengine hufika mbali hata kutaja kampuni wanayopenda kufanyia hiyo ajira. Sio mbaya sana ila ni hafifu inakupima kiasi gani kwenye maisha yako hujawahi fikiri kutawala na kumiliki. Mungu hakuumba watu mashuhuri na wasio mashuhuri aliumba wote sawa na kuwapa uwezo mbalimbali unaotofautiana........                "tu sawa lakini hatulingani" Tangu nimefahamu uwezo uliondani yangu sijawahi tamani kuwa flani, nasikitika kwa nini sikufahamu mapema uwezo nilionao. Leo ukiniuliza unataka kuwa nani nitakujibu nataka kuwa MIMI yaani vile nilivyojaaliwa na mwenyezi Mungu kuwa wapekee ndivyo niwe. Usiogope wewe pia una UWEZO.....Uwezo wako unaweza kuwa kwenye vidole vyako kama vile mimi ninavyochapa hili chapisho, unaweza kuwa kwenye miguu kama vile Lionel Messi anavyowa...

MWEZI WA NANE

Image
rethink MWANZO MPYA NA YESU KRISTO Neno mwanzo mpya linaweza kuwa ngumu kulielewa na nini kusudi LA kulifanya kuwa kichwa cha chapisho hili,namba ni mafumbo yaliyoanza tumika miaka mingi sana ulimwenguni. Namba ni viwakilishi vya vitu au mambo flani.Leo tuangazie kona ya biblia na namba pamoja na tafsiri yake, na tujikite kwenye namba inayowakilisha mwezi tulionao Wa nane. Namba nane inamaana kubwa kwa Mungu, mpaka kufanya mwanzo Wa juma uwe ni siku ya nane. Kila kitu katika biblia chenye mwanzo mpya kimefungamanishwa na namba nane. Mwezi Wa nane. Mwezi Wa nane ni mwezi unaosimama badala ya mwanzo, ufufuo, na ukombozi Wa mwanadamu kwa damu ya Yesu. (Kuzaliwa upya) Imenifurahisha kuona kuwa Leo ni jumatatu siku ya kwanza ya juma kwa wengi wetu na ni siku ya kwanza ya mwezi. Ila hii sio sababu halisi ya kuwa mwanzo mpya katika mwezi huu. Biblia inasema nini? Mungu aliokoa watu nane kwa safina kipindi cha gharika ya Nuhu, ili aanzishe uzao mpya ulimwenguni. Kama ilivy...

DREAM BIG_BIG DREAM

Image
Late: Martin Luther King didn't say that i have a plan , but he said "i have a dream" Here is the whole speech.... Martin Luther King's I have a dream speech August 28 1963                I am happy to join with you today in what will go down in history as the greatest demonstration for freedom in the history of our nation. Five score years ago, a great american, in whose symbolic shadow we stand today, signed the  Emancipation Proclamation . This momentous decree came as a great beacon light of hope to millions of Negro slaves who had been seared in the flames of withering injustice. It came as a joyous daybreak to end the long night of their captivity. But one hundred years later, the Negro still is not free. One hundred years later, the life of the Negro is still sadly crippled by the manacles of segregation and the chains of discrimination. One hundred years later, the Negro lives on a lonely island of poverty in ...