TEMBEA MBELE

Nilipokuwa nafikiria kuhusu mwezi wa tatu tulioanza leo nikakumbuka kitu kuhusu maana inayofanana na jina la mwezi huu. Mwezi wa tatu kwa kalenda ya Gregorian tunayotumia unaitwa kwa jina March, lenye maana yake kutokana na asili yake. Sikutaka kung’ang’ana na maana yake na asili yake ila nikafikiri kuhusu maana yake kwa lugha ya kimombo. March maana yake ni MWENDO. Tumetembea sana kwaajili ya mwenge, maadhimisho na mambo mengine mengi kama ishara ya kutiana hamasa. Mara nyingi kwenye matukio ya pamoja yanayogusa maisha ya kila mmoja watu huwa wanaandaa matembezi ya pamoja juu ya swala fulani. Lugha nyepesi wanaita maandamano ya amani, wengine wanasema matembezi kwaajili ya.......... kuna sababu kubwa moja ya msingi inayowafanya watu wafanya matembezi. Watu hufanya matembezi ili kujenga ufahamu kwa watu wote wanao kerwa na jambo hilohilo kuwa hawakopeke yao, ndio maana maandamano hayo hayana mwaliko. Mtu yeyote anaweza kuungana na kundi la watembezi kufanya wanachofa...