LATE MWALIMU NYERERE J.K LEGACY

rethink relive Mwalimu ni kiungo kikubwa cha maendeleo kama akijitambua na kutambulika na jamii husika yenye uhitaji huo. Mwalimu Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 April 13 kijijini Butongo, mzanaki huyu hakuwa mzanaki ilipofika wakati wa kupigania Uhuru na ukombozi. Hi heshima kubwa kushirikishana mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika kupigania Uhuru wa taifa na bara lote la Africa. Kiongozi ambaye maamuzi yake na hoja zake zilileta matokeo chanya kwa taifa. Alisaidia kuundwa kwa TANU Mwaka 1954 kuwa chama cha kisiasa jambo lililo mchukiza gavana wa uingereza Sir.Richard Gordon Turnbull. Alifanya maamuzi magumu ya kuacha kazi ya ualimu akiwa Mwalimu Pugu sekondari kama sehemu ya masharti aliyopewa na gavana kuwa achague moja kati ya siasa au kazi. Alishikiria maslahi ya wengi kuliko yake... "Niliogopa. Nikamuuliza Julius ikiwa ninachokisikia ni kweli, alipojibu ndio nikaogopa zaidi. Nikamwambia anachokifanya ni kibaya, Mungu amempa kazi unataka kuiha...