KANUNI 16 ZA KUISHI MAISHA YAKO.

rethink relive Habari yako ndugu msomaji wangu, wa mfululizo wa machapisho yanayogusa maisha yetu moja kwa moja hususani uwezo tulionao wanadamu wa kutufanya tuishi. Maisha yanakila kitu tunachotaka ila maisha hayatupi tunachotaka bali hutupa tunachotafuta kwa kuanza na kunia kupata. Leo tuangazie kona ya kuishi maisha yetu halisi, Tambua unawajibu wa kuishi maisha yako sio maisha ya mtu Fulani mashuhuri au mzazi wako. Maisha yetu yanaweza kutiwa hamasa na mtu ila sio kigezo cha kuishi kama yeye binafsi naita huo ni uvivu wa kufikiri. Hizi ni kanuni kumi sita za kuishi maisha yako. Penda kupenda . Upendo ni hali ya asili ila inataka utayari wa mtu husika, katika upendo mambo mengi yanafanikiwa, upendo ni dawa sio ya homa bali ya maisha kwa ujumla. Ndio maana vitabu vya kiimani imesisitiza sana, na kikristo upendo ni Mungu, yani Mungu ndio pendo. Ukitaka kuishi maisha yako kuna upendo unatakiwa kuwa nao, ni ule unaotokana na Mungu yani unaweza mpenda m...