Posts

Showing posts from June 3, 2016

MWEZI WA SITA

MWEZI WA SITA NI WA KUTUMIA MAMLAKA KUMSHINDA SHETANI Namba sita kwenye biblia inamaanisha udhaifu wa mtu na udhihirisho wa dhambi 27 Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba. 31 Mungu akatazama vyote alivyoumba na ilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita. SITA NI NAMBA YA MTU Kwasababu aliumbwa siku ya sita, na inabaki kuwakilisha kutokamilika kwetu. Ikumbukwe kuwa Mungu aliumba Mtu. Mtu bila Mungu atabaki kuwa asiyekamilika. Mungu akampulizia pumzi mtu naye akapata uhai. MTU HAJAKAMILIKA WALA HAJAWAHI KAMILIKA   Haijalishi kiasi gani tuna fanya jitihada kujikamilisha kwa nguvu zetu na maarifa, tunabaki kuwa chini ya namba saba namba ya ukamilifu. Licha ya kuto kamilika Mungu alivyoumba vyote akatazama na kuona vilikuwa ni vizuri sana. Inahitaji uweze kuona kama Mungu anavyokuona ndio utaweza kuona ukamilifu kwa njia ya neema ya Mungu. MTU ALIUMBIWA KA...