MWEZI WA SITA
MWEZI WA SITA NI WA KUTUMIA
MAMLAKA KUMSHINDA SHETANI
Namba sita kwenye biblia
inamaanisha udhaifu wa mtu na udhihirisho wa dhambi
27Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu
kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanaume na mwanamke
aliwaumba.
31Mungu akatazama vyote alivyoumba na ilikuwa
vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita.
SITA NI NAMBA YA MTU
Kwasababu aliumbwa siku ya
sita, na inabaki kuwakilisha kutokamilika kwetu. Ikumbukwe kuwa Mungu aliumba
Mtu. Mtu bila Mungu atabaki kuwa asiyekamilika. Mungu akampulizia pumzi mtu
naye akapata uhai.
MTU HAJAKAMILIKA WALA
HAJAWAHI KAMILIKA
Haijalishi kiasi gani tuna fanya jitihada
kujikamilisha kwa nguvu zetu na maarifa, tunabaki kuwa chini ya namba saba
namba ya ukamilifu.
Licha ya kuto kamilika Mungu
alivyoumba vyote akatazama na kuona vilikuwa ni vizuri sana. Inahitaji uweze
kuona kama Mungu anavyokuona ndio utaweza kuona ukamilifu kwa njia ya neema ya
Mungu.
MTU ALIUMBIWA KAZI KAMA
KUSUDI( A WORK IS ART OF BECOMING A TRUE BEING)
Siku ya sita inaonesha
kumalizika kwa kazi ya Mungu yaani uumbaji. Mungu akampa mtu kazi katika
bustani ya eden ili kuendeleza tamaduni ya kazi na sio laana kama mtazamo wa
wengi.
MTU KUPEWA MAMLAKA YA
KUTAWALA KABLA AJAUBWA SIKU YA SITA
26Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu,
wakatawale
juu ya samaki wa
baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe
wote watambaao juu ya nchi.’’
Licha ya udhaifu
tulionao Mungu ametupa mamlaka ya kutawala. shetani hana utawala bali ana nguvu
pekee, nguvu bila utawala uwezi fanya jambo. Utawala una mamlaka ndani yake.
Ndio maana TRA hawafanyi biashara yeyote ila wana mamlaka ya fedha ya nchi
yote, vivyo hivyo TCRA hawana chombo chochote cha mawasiliano ila wao ndio
wanasimamia mawasiliano.
Nyoka
aliyemdanganya mtu naye aliumbwa siku ya sita, ila alichokosa ni mamlaka juu ya
mtu.
Shetani anatuweza
pale tunapojaribu kujisahau na kutumia nguvu, bila mamlaka
SITA NAMBA YA
USAWA, USHIRIKIANO NA UPATANISHO
Muujiza wa kwanza
wa Yesu ulikuwa wa kubadilisha mitungi ya maji kuwa divai, kwenye sherehe ya DOA. Ndoa inamaanisha upatanisho.
Inaweza ikawa
sababu ya boaz kumpa ruthu vipimo sita
vya shayiri. Ruth 3:15
Kama tunapenda
mambo ya kimungu yatokee kwenye maisha
yetu tunatakiwa kukumbuka kuwa hatujakamilika pasipo Mungu. Tukubali kujazwa
mpaka juu kabisa kama mitungi ya maji, kama vile divai ilivyokuwa ajabu katika
harusi ya kana kadhalika maisha yetu.
My quote:-
And they overcame him by the blood of the Lamb,
and by the word of their testimony; and they loved not their lives unto the
death.
Written by: Mwakajila F.A
C.E.O
WORLD INSPIRATIONISM INC
’’inspired by God living to the limits of our
potential’’
Comments