Posts

Showing posts from March 7, 2017

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

Image
Kamusi sanifu inatoa maana ya thamani kuwa ni hali ya kuwa na faida, manufaa, kitu au mtu mwenye adili. Mtu yeyote anapenda kuwa wa thamani, mtu au kitu kuwa wa thamani inategemea sana matumizi yake na tabia yake, hasa tabia. Tabia ya kitu au mtu ndio hupelekea ubora wake kubaki kama ulivyo au kupungua. Hali na mazingira yanapobadilika kitu bora hubaki kama kilivyo na thanmani yake kuzidi kuongezeka. Chumvi ikichanganywa na mchanga utatafuta mbinu ya kuitoka kwenye mchanga ili uitumie, na ukiamua kwenda kuiuza chumvi hivyo iliyotolewa kwenye mchanga gharama yake haitakuwa ile ya mwanzo. Inaweza kuleta shida kidogo kujadili thamani ya mwanamke pekee wakati huo huo wote wawili mwanamke na mwanaume wanathamani sawa. Nafahamu kuwa wanaume wenzangu wanathamani sawa na mwanamke lakini ukiangalia leo duniani mwanamke huenda hajithamini au athaminiwi jamii yake. Chanzo kikubwa ni mwanamke yeye mwenyewe na ufahamu wake uliojaa mtazamo wa kusaidiwa na kutaka kuthaminiwa pasipo s...