KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

Habari ya uzima ndugu msomaji wangu, natumaini u mzima wa afya. Nimekuwa natamani kuandika kila mara, ningelikuwa mtoto mdogo ningechora kwenye mchanga. Leo tuangazie kuhusu kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa. Maneno haya yanabebana kimantiki licha ya kutofautiana katika matumizi. Kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa ni kati ya mambo yanayojitokeza kwenye maisha ya wengi wetu. KUJIKATAA;- Siku yako ya kwanza kufunguka ufahamu na kuelewa namna ulimwengu ulivyo ndio ulichukua hatua ya aidha kujikubali au kujikataa. Mungu ni fundi wa ajabu alitaka maisha yetu yote tuishi tukihamasishana kwa vile tulivyotofauti tofauti. Amempa mtu mmoja hekima mwingine busara sio kwamba mwenye hekima ajidharau kwa kukosa busara, ila waishi ulimwenguni wakijifunza na kubadilishana ujuzi. Mawazo ulioweka juu yako kuhusu hadhi uliyonayo, elimu,pesa, mwonekano na vingine, ndio yanapelekea ujenge mtazamo wa kujikataa. Inashangaza sana kuona akina Dada wana...