Posts

Showing posts with the label MAENDELEO BINAFSI

MASOMO 23 MWAKA 2017 UMENIFUNZA

Image
HamasikaLeo           Kama hauna ubunifu kila siku, upo  kwenye njia ya kurudi ulipotoka Tabia ya kuahirisha ni mbinu ya kukwepa kufanya vitu vipya. Usifanye kitu kama hakikupi furaha. Kama haujali sana basi haujakua sawasa. Kutokuwa na utulivu Wa mawazo ni ishara ya ukuaji. Kuwa mkarimu, mwenye matumaini, mwema na jasiri katika kila fursa ya maisha. Simu yako inakugharimu kesho yako. Wakati hakuna anayeamini maono yako unatakiwa kuwa mwaminifu kwa maono uliyonayo. Wakati mwingine kitu pekee chenye tija unachoweza kufanya ni kupumzika. Kazinia kusonga mbele badala ya kuwania ukamilifu. Jifunze kwa angalau saa moja kwa Siku, kufanya hivyo kutakufanya uone fursa ambazo wengi hawaoni na utashinda. Kufuta maneno dhaifu kama "siwezi" "haiwezekani" "ni ngumu" na kutumia maneno kama " hii ni nzuri" na " ngoja tujaribu". Kama ukimuhamasisha mtu mmoja kwa siku siku yako haijapotea. Kuishi kwenye historia yako ni kutoheshimu ke...

UNAWAZO GANI?

Image
Mwanzo wa kila kilichowahi kufanikiwa ni wazo, wazo lililobadilishwa na kuwa kitu halisi. Kabla hujawa na wazo hilo unatakiwa kuwa na picha ya wapi unataka kufika au nini unataka kufanya. Inakuwa bahati kama unapata mtu wa kukusaidia kuona picha yako kubwa kuhusu maisha yako, vinginevyo unatakiwa uone mwenyewe hiyo picha na utengeneze wazo la kukufikisha huko. Katika ulimwengu huu tunaoishi mawazo yatakayosaidia makundi makubwa ya watu ndio yanayoweza kushinda na kuishi kwa Muda mrefu.  Wengi wanaoanzisha mawazo huanzia kutoka kiwango cha chini na kuwa na mipango ya kupanda kuelekea juu hadi mawazo yanapowapeleka. Lakini kikwazo kikubwa kwa hili ni kwamba wengi wanaoanzia chini wanashindwa kuinua vichwa kuona FURSA zilizowazunguka kutokana na mawazo waliyonayo kwahiyo wanabaki na mawazo mazuri wakiwa chini. Inatakiwa kukumbuka kuwa mwonekano wa huko chini sio mzuri na unatabia ya kuua tamaa ya mambo makubwa unayoyaona. Wazo hutambuliwa kama chanzo cha utajiri, ...

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI

Image
Utangulizi Kukomboa muda ni dhana inayogusa watu wengi kwa maana kila mtu atamani siku moja awe mmiliki wa muda wake. Kukomboa muda sio sawa na kutunza muda, kama kuna kitu duniani kisichowezekana kutunzika ni muda pekee. Muda ulioutunza jana huwezi kuutumia leo. Unachoweza kufanya ni kutumia muda wote ulionao kwa kufanya mambo ya kimaendeleo, ndio ya kimaendeleo ikiwemo kulala! eeh namaanisha  maendeleo binafsi. Kuna wakati Unaweza kuwa  umesongwa na kazi nyingi lakini huzalishi kitu na haina maendeleo, je utakuwa umetumia muda vizuri? Sasa unatofauti gani na mtu aliyelala kwa maana ya kupumzika.  Unatumia muda, unatunza muda au unakomboa muda? Katika hayo matatu lenye ubora ni Kukomboa muda.  Ndio maana naandika kuhusu Kukomboa muda. Ukombozi ni dhana ya kimapinduzi inayobeba maudhui ya kujitoa kafara yani kujitoa sadaka.  Hizi ni mbinu za Ukombozi wa muda, kufanya hivyo utakuwa umejitoa sadaka kwaajili ya maisha yako, wengi wanaotumia mbinu ...

NEW YEAR RESOLUTION DON'T CHANGE YOUR CONFESSION

Image
HamasikaLeo Haujazeeka sana kiasi cha kughahiri malengo yako au kushindwa kuweka malengo mapya. Mambo mengine umekuwa  ukiyapanga na kupangua na kupanga kila mwaka bila mafanikio. Umekutana watu wanaojiita wahamasishaji kama huyu anayeandika na wamekufanya ujione kama hujawahi fanikiwa na kujisikia umechelewa na kukata tamaa. Ukipiga mahesabu ya mwaka 2016 hauoni fanikio la  kukufanya ufarijike na huenda ulipanga vizuri sana. Kuna ugonjwa fulani  wa mtu  kupanga kitu na unapofika muda wa utekelezaji hatekelezi mpaka muda unapita  na kupanga tena na tena, basi unakuwa  mchezo wa kupanga. Unajisikia ukakasi sana pale mwaka unapoisha hujafikia malengo yako au umefikia kwa kiwango hafifu. Wengi huwa tunabadili misimamo na kauli zetu tunapokutana na hali ya kutofikia malengo. Unaweza tumia mbinu hizo zinazoitwa mbinu za mafanikio na husionje hata harufu ya mafanikio na kuishia  kushawishika kukubaliana na hali halisi ya ugumu wa maisha. Takwim...

NAMNA YA KUKABILIANA NA MAWAZO YATOKANAYO NA HOFU.

Image
HamasikaLeo Habari za uzima ndugu msomaji wangu. Bado tuna endelea na harakati zetu za kujifunza namna ya kutumia uwezo wetu wote tulionao kufanya mambo duniani. Leo tujikite kwenye swala zima la  mawazo na hofu katika mchakamchaka wa kufukuzana na maendeleo ya mtu  kuanzia kwenye mawazo ya kila siku. Ni kanuni ya maisha ya kila binadamu kuwaza, shida inakuja pale mawazo yako yanapotawaliwa na hofu, na wakati mwingine kushindwa kutofautisha wazo linalotokana na hofu au Lisilo la hofu. Wengi tunaamua kuishi tu maisha yaendelee. Kama muda wote unawaza kiasi gani maisha yalivyo magumu kwako, muda wote utahisi kuwa wewe mi maskini kuliko wote. Hofu ya maisha na kujiona hujafanikiwa hakupelekei mambo mazuri kukujia. Kama unataka kubadilisha maisha yako, badili namna unavyofikiri....na vile unavyosema kwa sauti mbele ya watu. Je, unayowaza na kusema yanatokana na nini? Ni muhimu kufahamu kuwa haijarishi ni kiasi gani tatizo lako ni kubwa, ni kwa kiwango gani tatizo lim...

KANUNI 16 ZA KUISHI MAISHA YAKO.

Image
rethink relive Habari yako ndugu msomaji wangu, wa mfululizo wa machapisho yanayogusa maisha yetu moja kwa moja hususani uwezo tulionao wanadamu wa kutufanya tuishi. Maisha yanakila kitu tunachotaka ila maisha hayatupi tunachotaka bali hutupa tunachotafuta kwa kuanza na kunia kupata. Leo tuangazie kona ya kuishi maisha yetu halisi, Tambua unawajibu wa kuishi maisha yako sio maisha ya mtu Fulani mashuhuri au mzazi wako. Maisha yetu yanaweza kutiwa hamasa na mtu ila sio kigezo cha kuishi kama yeye binafsi naita huo ni uvivu wa kufikiri. Hizi ni kanuni kumi sita za kuishi maisha yako. Penda kupenda . Upendo ni hali  ya asili ila  inataka utayari wa mtu husika, katika upendo mambo mengi yanafanikiwa, upendo ni dawa sio ya homa bali ya maisha kwa ujumla. Ndio maana vitabu vya kiimani imesisitiza sana, na kikristo upendo ni Mungu, yani Mungu ndio pendo. Ukitaka kuishi maisha yako kuna upendo unatakiwa kuwa nao, ni ule unaotokana na Mungu yani unaweza  mpenda  m...

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

Image
Habari ya uzima ndugu msomaji wangu, natumaini u mzima wa afya. Nimekuwa natamani kuandika kila mara, ningelikuwa mtoto mdogo ningechora kwenye mchanga. Leo tuangazie kuhusu kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa. Maneno haya yanabebana kimantiki licha  ya kutofautiana katika matumizi. Kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa ni kati ya mambo yanayojitokeza kwenye maisha ya wengi wetu. KUJIKATAA;- Siku yako ya kwanza kufunguka ufahamu na kuelewa namna  ulimwengu ulivyo ndio ulichukua hatua  ya aidha kujikubali au kujikataa. Mungu ni fundi  wa ajabu alitaka maisha yetu yote tuishi tukihamasishana kwa vile tulivyotofauti tofauti. Amempa mtu  mmoja hekima mwingine busara sio kwamba mwenye hekima ajidharau kwa kukosa busara, ila  waishi ulimwenguni wakijifunza na kubadilishana ujuzi. Mawazo ulioweka juu  yako kuhusu hadhi uliyonayo, elimu,pesa, mwonekano na vingine, ndio yanapelekea ujenge mtazamo wa kujikataa. Inashangaza sana kuona akina Dada wana...

ACADEMIC EXCELLENCE AND LIFE IMPACTS🎓👑

30.03.2016 MOTIVATION SPEECH AT CASFETA TAYOMI ST.JOSEPH UNIVERSITY IN TANZANIA  OVERNIGHT ✔MOTIVATIONAL SPEAKER: DICKSON JOSHUA MKONGO ✔(M sc. Automation and Robotics, London) ✔(bachelor of Electronics and Communication Engineering, St.Joseph university in Tanzania 2010 as all time best student up to date) ACADEMIC EXCELLENCE AND LIFE IMPACTS🎓👑 INTRODUCTION 🔑There are different kinds of knowledge, the bible says that you will know the truth and truth will set you free. There is freedom which comes out of knowledge, apart from freedom of just because you are born again Christian. John 8:32 🔑 “You can’t change your yesterday but you don’t have to ruin your tomorrow make the most of everyday” 🔑 “You can’t change your destination overnight but you can change your direction overnight” Jim Rohn 🔑 “you can’t make change that instantly but today’s decision can change direction, and you will succeed if you won’t change the decision.” 🔑Before the Glory comes sufferin...