MASOMO 23 MWAKA 2017 UMENIFUNZA

HamasikaLeo

         
  1. Kama hauna ubunifu kila siku, upo  kwenye njia ya kurudi ulipotoka
  2. Tabia ya kuahirisha ni mbinu ya kukwepa kufanya vitu vipya.
  3. Usifanye kitu kama hakikupi furaha.
  4. Kama haujali sana basi haujakua sawasa. Kutokuwa na utulivu Wa mawazo ni ishara ya ukuaji.
  5. Kuwa mkarimu, mwenye matumaini, mwema na jasiri katika kila fursa ya maisha.
  6. Simu yako inakugharimu kesho yako.
  7. Wakati hakuna anayeamini maono yako unatakiwa kuwa mwaminifu kwa maono uliyonayo.
  8. Wakati mwingine kitu pekee chenye tija unachoweza kufanya ni kupumzika.
  9. Kazinia kusonga mbele badala ya kuwania ukamilifu.
  10. Jifunze kwa angalau saa moja kwa Siku, kufanya hivyo kutakufanya uone fursa ambazo wengi hawaoni na utashinda.
  11. Kufuta maneno dhaifu kama "siwezi" "haiwezekani" "ni ngumu" na kutumia maneno kama " hii ni nzuri" na " ngoja tujaribu".
  12. Kama ukimuhamasisha mtu mmoja kwa siku siku yako haijapotea.
  13. Kuishi kwenye historia yako ni kutoheshimu kesho yako.
  14. Sema "samahani" kuonesha kuheshimu, sema " asante" kuonesha kukubali.
  15. Ni heri kuwahi saa moja kabla, kuliko kuchelewa dakika moja.
  16. Mtu anayetaka kufanya vyote hafanikishi kitu, Lenga... Lenga....
  17. Tafakari kila siku juu ya wewe, acha kuchangamkia teknolojia  kila siku.
  18. Tabia yako ya kila siku inatangaza imani yako ya kweli.
  19. Maumivu yatokanayo na historia yako yanaweza kutumika kama hazina ya hekima, kukua, ubunifu na tija kwaajili ya kesho.
  20. Kwa mtu mwaminifu; inagharimu miaka 30 kujenga sifa ni sekunde 30 tu zinatosha kupoteza sifa hiyo.
  21. Kuwa simba sio kondoo, kuwa mshindi sio muhanga.
  22. Nafuu ina gharama.
  23. Tumia sehemu iliyobaki ya maisha yako kama ushuhuda utakao saidia wengine.

Team Inspiration Inc tumejipanga kubadilisha maisha ya watu kuanzia kwenye mitazamo na mwaka2018 ni wako.
2018 Lenga Shabaha


Mwakajila Frank
Mwandishi.


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI