AMSHA MOYO WA SIMBA NDANI YAKO.

Ikiwa ni miaka kadhaa tangu uwepo duniani umewahi jiuliza umewahi fanikisha mambo mangapi, Kama hujawahi Leo unaweza jifunza kitu kipya au Kama umefanikisha leo unaweza kuongeza kitu kwenye Ufahamu wako. Siri moja wapo ya kufanikisha kitu ni kuwa simba wa eneo linalokuzunguka, simba angurumaye kwa ujasiri na nguvu akiamini hakuna simba mwingine eneo analoishi au eneo la kazi anayoifanikisha. Simba akinguruma sauti yake husikika zaidi ya kilomita 8. Mara nyingi watu wamemtumia kuonesha nguvu na ujasiri katika kazi zao. Simba sio mnyama mkubwa kuliko wote Wala Sio mwenye nguvu kuliko wote mwituni, lakini amepewa jina la kuitwa mfalme wa mwituni. Ukimfatilia kwa Karibu simba ni mnyama anayetumia muda mrefu kupumzika na kundi dogo la familia, kwajina lingine anaonekana kuwa ni mvivu sana. Simba awindaye mara zote huenda na mwenzake au wenzake wawili ila sio kwa pamoja bali ni kwa kunyata kwa ujanja mwingi. Leo tujikite kujifunza tabia za mtu mwenye kufanikisha jambo kup...