TISA DISEMBA NA UHURU WA FIKRA

" Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa fikra " moja ya nukuu za Hayati Mwalimu Nyerere JK. Akimaanisha umaskini unaotokana na fikra za kitumwa, kushindwa au kutopewa fursa ya maamuzi juu ya hatma yako, kuwepo duniani kwa lengo la kuongeza idadi ya raia na si huru kama wengine. "Hakuna anayeweza kukutawala bila kuanzia kwenye ufahamu wako" utawala mzuri na makini unaanzia kwenye fahamu yani kukufanya utengeneze fikra ya kuwa mtumwa na uwe umeridhika na kutumika. Siku hizi neno zuri ni Mtumishi( ina maana sawa na mtumwa wakati mwingine lina maanisha mfuasi). Uhuru una maana halisi ya kuwa na haki ya maamuzi binafsi bila ya kuingiliwa na mtu au taifa lingine. Huwezi kufanya maamuzi yako bila kuhusisha fikra. Kwa maana hiyo mwenye Uhuru Wa fikra pekee ndio raia huru kweli na si vinginevyo. " Mtumwa hata akipewa haki ya kuamua atafanya kama anavyofikiri Bwana wake." Uhuru tuliona...