TISA DISEMBA NA UHURU WA FIKRA
"Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa fikra" moja ya nukuu za Hayati Mwalimu Nyerere JK. Akimaanisha umaskini unaotokana na fikra za kitumwa, kushindwa au kutopewa fursa ya maamuzi juu ya hatma yako, kuwepo duniani kwa lengo la kuongeza idadi ya raia na si huru kama wengine.
"Hakuna anayeweza kukutawala bila kuanzia kwenye ufahamu wako" utawala mzuri na makini unaanzia kwenye fahamu yani kukufanya utengeneze fikra ya kuwa mtumwa na uwe umeridhika na kutumika. Siku hizi neno zuri ni Mtumishi( ina maana sawa na mtumwa wakati mwingine lina maanisha mfuasi).
Uhuru una maana halisi ya kuwa na haki ya maamuzi binafsi bila ya kuingiliwa na mtu au taifa lingine. Huwezi kufanya maamuzi yako bila kuhusisha fikra. Kwa maana hiyo mwenye Uhuru Wa fikra pekee ndio raia huru kweli na si vinginevyo.
"Mtumwa hata akipewa haki ya kuamua atafanya kama anavyofikiri Bwana wake."
Uhuru tulionao unatakiwa kuwa na chachu ya ongezeko la kasi ya ukuaji wa uchumi, elimu(sayansi na teknolojia), siasa na ustawi wa jamii. Ongezeko hilo ndio ishara ya kuwa tuna maamuzi yetu wenyewe kama nchi huru na tunajitegemea kiuchumi,kisiasa na kiutawala, kielimu kwa maana ya sayansi na teknolojia na kijamii. Je, Ni kweli tunajitegemea? Au tunaendelea kujikomboa kutoka utumwani? ItaƧhukua muda gani? Kuna mikakati gani ya kukomboa watanganyika wote kwa maana ya watanzania kwa sasa?
Kama mtanzania najivunia na kuenzi jitihada za waasisi wa taifa la Tanganyika na Tanzania kwa ujumla maana kazi yao ilikuwa ndio mwanzo wa ukombozi wa fikra za watu wa Tanzania.
Mtanzania anayependa maendeleo hato acha kutamani uongozi wa serikali kuu na ndogo pamoja na mihimili ya bunge na mahakama kuwa ni huru na inayotenda haki. Huru maana yake isiyoingiliwa kimaamuzi kutoka nje au ndani ya nchi bali kwa kufuata misingi ya katiba.
Ni makosa makubwa mtanzania kusema tulipata Uhuru Wa bendera, na ukosefu wa maarifa juu ya kile tunachokiita tisa Desemba. Nikimnukuu mwanasiasa mwanamke wa kwanza kugombea urais Tanzania Mh. Anna Mghirwa akiwa kwenye harakati za kutapatapa kuhamia CCM hapo Jana kwenye mkutano Wa UWT alisema,"Siasa ya Tanzania inabadilikabadilika" nilivyoelewa ni kwamba alikuwa anajitetea tu, na ukweli ni kwamba kama inabadilika ni vyema na ndio jambo jema. Ila swali litabaki palepale inabadilika kutoka wapi kwenda wapi? Ikiwa inakua ni vyema ila kama inadumaa kwa maslahi ya watu wachache, hilo ni tatizo.
Ni jukumu letu la kwanza la kiuzalendo kupigania Uhuru wa taifa letu kuanzia fikra na mitazamo tuliyonayo. Hii ni kiwezesha kupata Uhuru Wa kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kielimu na kijamii.
Na
Mwakajila Frank
Mwandishi
Team Inspiration Inc.
Comments