FUNGUO 5 ZA MAAMUZI

Kila mtu ni mfanya maamuzi. Tunategemea taarifa na mbinu za kutuwezesha kufanya hayo maamuzi na hapo ndio maamuzi yanapotofautiana baina yetu. Tunapokwenda mgahawani, orodha ya chakula ndio inayotupa nafasi ya kufanya maamuzi kwa kutupa taarifa sahihi za chakula kilichopo mahali hapo. Orodha hiyo ya chakula inafika mbali kwa kutupa gharama ya kila chakula tukakacho kula, hivyo kuweza kupima gharama ya matumizi yetu kabla ya kutumia. Kufanya jambo lolote ia kunahitaji kufanya maamuzi, kwenye biashara, kazi hadi siasa inahitaji maamuzi ya awali. Uamuzi unafanyika katika hali ya kutokuwa na uhakika, wakati ujao haujulikani na wakati mwingine wakati uliopita hali yake ni ya makisio tu. Chapisho hili linaweza kukusadia kukupa mbinu za kukusaidia kuhimiza uwezo wako wa kufanya maamuzi katika ulimwengu tulionao ambao mambo mengi hayanauhakika, hubadilika badilika na wakati mwingine hali nyingine zinazoweza jitokeza zisiz...