FUNGUO 5 ZA MAAMUZI
Kila mtu ni mfanya
maamuzi. Tunategemea taarifa na mbinu za kutuwezesha kufanya hayo maamuzi na
hapo ndio maamuzi yanapotofautiana baina yetu. Tunapokwenda mgahawani, orodha
ya chakula ndio inayotupa nafasi ya kufanya maamuzi kwa kutupa taarifa sahihi
za chakula kilichopo mahali hapo. Orodha hiyo ya chakula inafika mbali kwa
kutupa gharama ya kila chakula tukakacho kula, hivyo kuweza kupima gharama ya
matumizi yetu kabla ya kutumia. Kufanya jambo lolote ia kunahitaji kufanya
maamuzi, kwenye biashara, kazi hadi siasa inahitaji maamuzi ya awali.
Uamuzi unafanyika
katika hali ya kutokuwa na uhakika, wakati ujao haujulikani na wakati mwingine
wakati uliopita hali yake ni ya makisio tu. Chapisho hili linaweza kukusadia kukupa
mbinu za kukusaidia kuhimiza uwezo wako wa kufanya maamuzi katika ulimwengu
tulionao ambao mambo mengi hayanauhakika, hubadilika badilika na wakati
mwingine hali nyingine zinazoweza jitokeza zisizoweza kuzuilika.
Ongeza chaguzi zako
Kuamua kunatanguliwa na
kitendo cha kuchagua kwanza, kabla haujaamua ninauhakika unakuwa na mambo mbele yako na unataka kufanya moja kwanza au moja tu na kuachana na mengine
yote. Unachotakiwa ni kuongeza uwanja wa mambo unayoyachagua kabla haujaanza
kuyapunguza moja baaada ya linguine. Ukiwa na machagulio mawii tu unakuwa na
uwanja mdogo wa kuamua. Ni kweli inafika wakati mambo ya kuchagua yawe machache
ndio urahisi unakuja, yatakuwaje machache kabla hayajawa mengi?
Jaribu machagulio yako
kabla haujabaki na chaguzi moja.
Chaguzi zako nyingi
zitafutie taarifa sahihi kwanza zote kwa usawa, usiwe na upendeleo wa kitu
kimoja kwanza kabla ya kuchunguza vyote. Tatizo hili kinawakumba wengi sana kwa
kuwa na upendeleo wa machagulio waliyonayo. Unataka kufanya biashara na una
mawazo matan ya biashara, kati ya hayo matano tafuta taarifa sahihi kwa usawa
juu ya mawazo yote. Mwisho utafikia hatua ya kuamua moja la kufanya au mawili
kulingana na ulivyopanga.
Epuka mihemko ya muda
mfupi.
Tumia
kanuni ya 10/10/10 baada ya dakika 10 utajisikiaje kuhusu
maamuzi hayo, vip kuhusu baada ya miezi 10? Na vip kuhusu miaka 10? Epuka kupotezwa
katikati ya hisia za muda mfupi zinazokupa mihemko ya muda mfupi na kukuacha
ukiwa unajuta. Maamuzi mazuri ni yale ambayo matunda yake yanadumu kwa muda
mrefu kufaidisha maisha yako yote.
Jiandae kukosea kufanya
maamuzi.
Ni jambo la ajabu kujiandaa
kukosea kufanya kitu wakati umefanya kwa uhakika. Mamuzi ni jambo la kuweka
uhakika pasipo na uhakika. Tatizo letu wengi tunapokuwa tunafanya maamuzi
tunasahau kama mwanzoni yalikuwa makisio ya jambo na kuweka imani zetu zote
hapo, sio kila maamuzi mazuri unayofanya lazima yafanikiwe na sio kila maamuzi
ambayo hayakufanikiwa hayakuwa mazuri. Hatua za mwanzo zikikosewa kufuatwa hii
hatua ya nne lazima itajitokeza. Kukosea maamuzi kunafanya wafanyabiashara
wafirisike, wafanyakazi wafukuzwe kazi lakini wote bado wanatakiwa kujiandaa
kwa hayo yote.
Kuwa tayari kubadili
maamuzi
Ukiwa na kitu unatamani
kwenye maisha huwezi shindwa kuwa tayari kubadili maamuzi yako. Kanuni ya shauku+uamuzi×nia=hatma
inaeleza wazi kuwa maamuzi ndio yenye uwezekano mkubwa wa kubadilika. Maamuzi ndio
yenye uwezo wa kuathiri maisha yako yote yaani hatma yako ikawa sivyo
ulivyotegemea.
Msimamo wa kimaamuzi ni
muhimu kwa kila mtu kwasababu kila mtu ni mfanya maamuzi. Ufasaha wa maamuzi
ndio ufasaha wa mipango yako na ndio hatua za kufanikisha mambo unayofanya. Uwe
na uhakika kuwa unafanya maamuzi kwaajili ya maisha yako na maisha yako
yatakuwa vile unavyoenda yawe. Mara zote tunavunjika moyo kwasababu tuna
matarajio mengi kuhusu maamuzi yetu na yanaokuja tofauti tunashindwa
kukubaliana na matokeo, huu usiwe mwisho wa kuendelea kufanya maamuzi sahihi.
Frank mwakajila
Mwandishi.
Comments