KUWA WEWE

rethink KUWA WEWE umewahi jiuliza unapenda kuwa nani kwenye maisha yako? au umewahi kuulizwa unapenda kuwa nani kwenye maisha yako?, wengi hutoa majibu ya ajira wanazopenda na wengine hufika mbali hata kutaja kampuni wanayopenda kufanyia hiyo ajira. Sio mbaya sana ila ni hafifu inakupima kiasi gani kwenye maisha yako hujawahi fikiri kutawala na kumiliki. Mungu hakuumba watu mashuhuri na wasio mashuhuri aliumba wote sawa na kuwapa uwezo mbalimbali unaotofautiana........ "tu sawa lakini hatulingani" Tangu nimefahamu uwezo uliondani yangu sijawahi tamani kuwa flani, nasikitika kwa nini sikufahamu mapema uwezo nilionao. Leo ukiniuliza unataka kuwa nani nitakujibu nataka kuwa MIMI yaani vile nilivyojaaliwa na mwenyezi Mungu kuwa wapekee ndivyo niwe. Usiogope wewe pia una UWEZO.....Uwezo wako unaweza kuwa kwenye vidole vyako kama vile mimi ninavyochapa hili chapisho, unaweza kuwa kwenye miguu kama vile Lionel Messi anavyowa...