KUWA WEWE
rethink
KUWA WEWE
KUWA WEWE
umewahi jiuliza unapenda kuwa nani kwenye maisha yako? au umewahi
kuulizwa unapenda kuwa nani kwenye maisha yako?, wengi hutoa majibu ya ajira
wanazopenda na wengine hufika mbali hata kutaja kampuni wanayopenda kufanyia
hiyo ajira. Sio mbaya sana ila ni hafifu inakupima kiasi gani kwenye maisha
yako hujawahi fikiri kutawala na kumiliki. Mungu hakuumba watu mashuhuri na wasio
mashuhuri aliumba wote sawa na kuwapa uwezo mbalimbali unaotofautiana........
"tu sawa lakini hatulingani"
Tangu nimefahamu uwezo uliondani yangu
sijawahi tamani kuwa flani, nasikitika kwa nini sikufahamu mapema uwezo
nilionao. Leo ukiniuliza unataka kuwa nani nitakujibu nataka kuwa MIMI yaani
vile nilivyojaaliwa na mwenyezi Mungu kuwa wapekee ndivyo niwe. Usiogope wewe
pia una UWEZO.....Uwezo wako unaweza kuwa kwenye vidole vyako kama vile mimi
ninavyochapa hili chapisho, unaweza kuwa kwenye miguu kama vile Lionel Messi
anavyowashangaza wengi, unaweza kuwa kwenye mikono kama Dr.Benjamin Carson.Sr.
kuna maana nyingi za mafanikio leo
tuangalie hii moja niliyojifunza kutoka kwa mwandishi wa THE RICHEST MAN IN
BABYLON, George.S.Clason katika maneno yake ya utangullizi ameandika,
" mafanikio ni kutimia kwa jambo kama matokeo ya jitihada zetu na uwezo
tulionao". Kutimia, jitihida, uwezo na matokeo ni maneno muhimu kwenye
maana hiyo.
JITIHADA;- ni dhamira ya dhati katika kufanya jambo.
KUTIMIA;- ni ukamilifu wa jambo linalifanywa.
MATOKEO;- hali inayoonekana baada ya jambo kukamilika
UWEZO;- ni nguvu kazi inayopelekea jambo linalitakiwa kutimia
litimie.
Kimsingi dunia yote hatuwezi tukawa mabilionea au watu washuhuri,
lakini tunaweza kuwa angalau wazazi wa watu mashuhuri wajao. Mark zuckerberg mjasiriamali
wa mtandao ni tajiri wa tano kwa sasa ulimwenguni akiwa na umri wa miaka 32,
wengi tunaweza sema amepata zali la kugundua programu ya kompyuta, la hasha
kakuna kitu kinaitwa zali kwenye sayari ya dunia. Mazingira na wazazi wake wamechangia
yeye kufika pale alipo kwasababu walitambua UWEZO wake alionao………Matajiri wa
Africa hawawezi elezea utajiri wao wazi sifahamu kwanini, ila naamini wao pia
wametumia UWEZO wao wa ndani….
Nikisema uwezo wangu au wako ni kwamba vile ulivyojaaliwa kufanya
ambavyo hakuna mtu duniani anafanya, nikisema hakuna,ni hakuna kweli na hajawahi kutokea. Kama wewe ni
fundi viatu na ukashona viatu kama kazi ya mikono unayoipenda sio kwasababu
usipofanya njaa itakumaliza, hakika utashona kiasi cha kutoweza kufananishwa na
mtu yeyote duniani….
Uwezo wako ulionao ndio utakufanya uwe tofauti na wengi sana
wanaokuzunguka. Nakataa na ninakusaidia kukataa kuwa tunalingana, anayelingana
na wewe hajazaliwa bado, atazaliwa pale utakapokubali kushindwa…kushindwa
kutambua uwezo ulionao. Ben carson MD kwenye kitabu chake cha “mikono
iliyozawadiwa” ameandika…
<sio
nini unafanya, ila namna unavyofanya kazi unayofanya ndio unaweza leta utofauti”>…..
Wakati mwingi ninapenda kukaa peke yangu na kuanza kujitathmini mwenyewe
nikijiweka kizimbani na kujihoji, kujikosoa na kujikumbusha mikakati. Muda wako
wewe na mtu wako wa ndani utakusaida KUJITAMBUA NA KUJIENDELEZA. Kuna watu
wanavito vya thamani kwenye miili yao na hata sasa hawajavitambua, inawezekana
sauti, hekima, uongozi,mwonekano,elimu na vingine vingi vinaweza kuwa na uwezo.
Ni huzuni sana kama hutaweza kutambua uwezo wako mpaka mauti ikufike maana itakuwa
hasara kwa ulimwengu wote kupoteza tunu yenye thamani iliyondania yako…………itaendelea
Nukuu yangu:-
“Potential and success are married unless ignorance proclaim
divorce”
Frank Mwakajila,
C.E.O,
World Inspiration Inc.
Inspired by God living to the limits of our potential.
Comments