KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

Habari ya uzima ndugu msomaji wangu, natumaini u mzima wa afya. Nimekuwa natamani kuandika kila mara, ningelikuwa mtoto mdogo ningechora kwenye mchanga.

Leo tuangazie kuhusu kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa. Maneno haya yanabebana kimantiki licha  ya kutofautiana katika matumizi. Kujikataa, kukataliwa na kukata tamaa ni kati ya mambo yanayojitokeza kwenye maisha ya wengi wetu.


KUJIKATAA;-
Siku yako ya kwanza kufunguka ufahamu na kuelewa namna  ulimwengu ulivyo ndio ulichukua hatua  ya aidha kujikubali au kujikataa. Mungu ni fundi  wa ajabu alitaka maisha yetu yote tuishi tukihamasishana kwa vile tulivyotofauti tofauti. Amempa mtu  mmoja hekima mwingine busara sio kwamba mwenye hekima ajidharau kwa kukosa busara, ila  waishi ulimwenguni wakijifunza na kubadilishana ujuzi.

Mawazo ulioweka juu  yako kuhusu hadhi uliyonayo, elimu,pesa, mwonekano na vingine, ndio yanapelekea ujenge mtazamo wa kujikataa. Inashangaza sana kuona akina Dada wanaweka makalio, matiti, nywele na sura za bandia wakati wanavyo vyote. Tusifike mbali kuwahukumu kuwa ni machukizo mbele za muumba( Mungu) ila  kisaikolojia tu ni hali  ya kutojikubali.

Binadamu tunatabia fulani isiyo mpendeza Mungu na wanadamu, tunabadili uongo kuwa ukweli ili kukidhi hamu, haja na kiu  tulizonazo, ambazo ni mlundikano wa tamaa. Ashukuriwe Mungu kuwa yeye ni Mungu na sio mwanadamu maana angetuangamiza.

Unapofika hatua  ya kujitambua kuna hatua  tumeiona hiyo ya kujikataa. Pamoja na hiyo zipo nyingine ambazo ni;-

  1. Kujitambua na kubadili ukweli.
  2. Kujitambua na kukubali ukweli.
  3. Kujitambua na kukata tamaa.
Tutaziona hizo mbili kadri tukiendelea pamoja. Kimsingi ni kwamba katika kukua na kujitambua kunaenenda katika njia kuu tatu ambazo hutupa watu wa aina tatu.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wengi wakishajitambua mapungufu yao  ghafla wanatafuta namna  ya kujifanya kuwa hawana mapungufu yeyote. Walio kwenye mahusiano ya aina  yeyote wanaweza kuwa shahidi zangu hapo, iwe ni ofisini, ndoa au ndugu.

Kujitambua na kukubali ukweli.
Kundi dogo la  watu hujitambua na kukubaliana na huo udhaifu, na kutambua kuwa sio kila eneo la  maisha yao  ni dhaifu. Nguvu kubwa wanaihamishia kule  ambako sio dhaifu na kushinda katika mambo mengi. 

Ukweli ni kwamba mwanadamu ameumbwa na uwezo, sio kila eneo uwezo wako unafanana, kuna baadhi ya vitu unaweza  zaidi na vingine huwezi kwa kiwango kizuri. Si kwamba huwezi kabisa ila  unazidiwa na wengine. Maisha ni mashindano ya hiari, wavivu wa kufikiri ndio wanaangalia ukweli na kukata tamaa ila  wanaojitambua hawaondoki eneo la  mashindano.

KUKATALIWA
hofu ya wengi ni kukataliwa, atanifikiriaje? Sijui amevutiwa na Mimi? Ngoja nijaribu ila  mmmmh? Hayo ni maswali ya vijana wengi wanaotaka kuanzisha mahusiano. 

Tatizo sio hofu Bali ni kujitambua, sio kosa kujitambua kuwa wewe huna pesa, elimu, hadhi, mwonekano mzuri  na vingine vinavyoumiza akili  yako, ila una amua nini baada ya kujitambua? Kabla ya kupeleka CV yako kwenye kampuni unafikiria nini kuhusu wewe? Kabla ya kuanzisha biashara yako unajithaminishaje wewe na bidhaa yako au huduma.



Kwa kweli ukijikataa na kubaki hivyo hivyo hakuna atakaye kukubali daima, usidanganywe na movies za kikorea au kifilipino mama, baba na vijana wenzangu. Umejiandaaje pindi unapokataliwa? Tena ukiwa hauna plan B. Siku zote wenzangu wanaojua kuishi ndoto zao huwa hawana plan B wala  njia mbadala, tatizo kubwa hilo!!!!

Tafiti zinaonesha wengi waliowahi kataliwa Mara nyingi  na kubaki na misimamo waliyonayo hufika mbali katika ndoto zao na kushinda. 
" Nawashukuru watu waliowahi nikatalia, kwasababu pindi walipokataa ndio niliweza kufanya mwenyewe " Be. Albert Einstein.

Tafiti zinaonesha kuwa watu mashuhuri waliowahi kuishi duniani walikuwa na misimamo mikali kwa mambo wanayoyaamini na kuyafanya. Usikubali watu wakuelewe kwa kila kitu kwa haja ya kuogopa kukataliwa, kaza mwendo songa mbele watakuelewa mbele ya safari.

KUKATA TAMAA
Hatua ya tatu ya mtu  aliyejitambua kuwa anamadhaifu baada ya kujikataa au kukataliwa anaishia kukata tamaa. Kama kukata tamaa ni jambo zuri  ulimwengu  huu usingekuwa hivi ulivyo hata robo.

Umewahi tembea ulimwenguni au hata kupitia mitandao na kuona jinsi miji ilivyojengwa, mahali pengine imejengwa kwa kuchonga miamba kipindi hicho hakukuwa na technolojia ni nguvu za watu waliohamasika na kusahau upande wa pili wa shilingi kuwa haiwezekani. 

Mfano wa mama anayekaribia kujifungua na akaghaili uzazi na kuomba wahalibu mimba hiyo. Tofauti yetu na huyo mama ni kwamba tunaishi kwenye dunia ambayo mambo mazuri hayazungumzwi kabisa, tunawaza vitu vidhaifu kila iitwapo leo. Kama tungekuwa na macho ya kuona uhalisia watu tungekuwa sio wa kukata tamaa.

Mpenzi usifanye haraka  kukata tamaa kwa jambo unaloliota,unalolifanya au kuwaza.

"Ndoto sio jambo unaloliona kipindi umelala Bali ni lile  linalokunyima usingizi".

Je, umewahi kosa usingizi kwa jambo lako? Jibu lako likufanye ukakamae na kusonga mbele. Usitafutize vijisababu visivyokuwa na maana ili kutete udhaifu wako. Tafuta nguvu zako zilipo kwenye mwili wako na zitakupa Furaha maishani  mwako. Binafsi ninavyoandika najihisi furaha  nadhani nguvu zangu zipo kwenye vidole vyangu vya mikono, licha ya madhaifu mengi niliyonayo nasonga mbele nikijua nimeshinda yote.
Itaendelea..........
Na;-
Mwakajila Frank.
C.E.O.
World Inspiration Inc
"Inspired by God living to the limits of our potential."




Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI