UNAWAZO GANI?

Mwanzo wa kila kilichowahi kufanikiwa ni wazo, wazo lililobadilishwa na kuwa kitu halisi. Kabla hujawa na wazo hilo unatakiwa kuwa na picha ya wapi unataka kufika au nini unataka kufanya. Inakuwa bahati kama unapata mtu wa kukusaidia kuona picha yako kubwa kuhusu maisha yako, vinginevyo unatakiwa uone mwenyewe hiyo picha na utengeneze wazo la kukufikisha huko. Katika ulimwengu huu tunaoishi mawazo yatakayosaidia makundi makubwa ya watu ndio yanayoweza kushinda na kuishi kwa Muda mrefu. Wengi wanaoanzisha mawazo huanzia kutoka kiwango cha chini na kuwa na mipango ya kupanda kuelekea juu hadi mawazo yanapowapeleka. Lakini kikwazo kikubwa kwa hili ni kwamba wengi wanaoanzia chini wanashindwa kuinua vichwa kuona FURSA zilizowazunguka kutokana na mawazo waliyonayo kwahiyo wanabaki na mawazo mazuri wakiwa chini. Inatakiwa kukumbuka kuwa mwonekano wa huko chini sio mzuri na unatabia ya kuua tamaa ya mambo makubwa unayoyaona. Wazo hutambuliwa kama chanzo cha utajiri, ...