NEW YEAR RESOLUTION DON'T CHANGE YOUR CONFESSION

HamasikaLeo Haujazeeka sana kiasi cha kughahiri malengo yako au kushindwa kuweka malengo mapya. Mambo mengine umekuwa ukiyapanga na kupangua na kupanga kila mwaka bila mafanikio. Umekutana watu wanaojiita wahamasishaji kama huyu anayeandika na wamekufanya ujione kama hujawahi fanikiwa na kujisikia umechelewa na kukata tamaa. Ukipiga mahesabu ya mwaka 2016 hauoni fanikio la kukufanya ufarijike na huenda ulipanga vizuri sana. Kuna ugonjwa fulani wa mtu kupanga kitu na unapofika muda wa utekelezaji hatekelezi mpaka muda unapita na kupanga tena na tena, basi unakuwa mchezo wa kupanga. Unajisikia ukakasi sana pale mwaka unapoisha hujafikia malengo yako au umefikia kwa kiwango hafifu. Wengi huwa tunabadili misimamo na kauli zetu tunapokutana na hali ya kutofikia malengo. Unaweza tumia mbinu hizo zinazoitwa mbinu za mafanikio na husionje hata harufu ya mafanikio na kuishia kushawishika kukubaliana na hali halisi ya ugumu wa maisha. Takwim...