NEW YEAR RESOLUTION DON'T CHANGE YOUR CONFESSION
HamasikaLeo
Haujazeeka sana kiasi cha kughahiri malengo yako au kushindwa kuweka malengo mapya. Mambo mengine umekuwa ukiyapanga na kupangua na kupanga kila mwaka bila mafanikio. Umekutana watu wanaojiita wahamasishaji kama huyu anayeandika na wamekufanya ujione kama hujawahi fanikiwa na kujisikia umechelewa na kukata tamaa. Ukipiga mahesabu ya mwaka 2016 hauoni fanikio la kukufanya ufarijike na huenda ulipanga vizuri sana.
Kuna ugonjwa fulani wa mtu kupanga kitu na unapofika muda wa utekelezaji hatekelezi mpaka muda unapita na kupanga tena na tena, basi unakuwa mchezo wa kupanga. Unajisikia ukakasi sana pale mwaka unapoisha hujafikia malengo yako au umefikia kwa kiwango hafifu.
Wengi huwa tunabadili misimamo na kauli zetu tunapokutana na hali ya kutofikia malengo. Unaweza tumia mbinu hizo zinazoitwa mbinu za mafanikio na husionje hata harufu ya mafanikio na kuishia kushawishika kukubaliana na hali halisi ya ugumu wa maisha.
Takwimu zinasema ni 8% tu ya watu wanaopanga kuhusu mwaka wanafikia malengo yako ya mwaka, kama umefikia malengo basi utakuwa ndani ya asilimia hiyo kama ni muhanga basi piga moyo konde.
Maazimio ya mwaka mpya sio lazima yawe makubwa kama unavyofikiria inaweza kuwa kupungua uzito, kubadili mtindo wa maisha au hata kubadili kazi unayofanya. Mambo haya na mengine mengi yanafungwa ndani ya muda ndio maana watu huwa wanayapangia mkakati.
Azimio la mwaka halifanyiki ili kukufanya ubadilike kama namba ya mwaka inavyobadilika, ukifanya hivyo utakuwa mtu wa kubadilika tu bila matokeo.
Kanuni saba za kuweka maazimio ya mwaka mpya
Kwa mtazamo wa saikolojia ya tabia ya binadamu hizi ni kanuni saba kuu za kukufanya upange maazimio ya Mwaka mpya na kutazamia kufanikiwa.
Maazimio dhahiri/maalumu
Kuna wakati unaweka maazimio ambayo sio halisi na una uhakika kuwa hayawezi kufanikiwa. Na hujawa na tabia ya msingi ya kukupeleka huko unapotaka kwenda. Maazimio kuwa dhahiri, kuweza kupimika, kuwezekana kutimia, kuwa halisi na kufungwa na muda ni mwanzo mzuri wa kutimia kwake.
Kupima maendeleo
Kama unaweza kupima maendeleo unaweza kubadili namna ya kufikia ukiwa njiani kutimiza maazimio hayo kama ikitokea changamoto njiani. Hii hutoa mwitikio ambao hukupa hamasa Mara unavyoangalia ulipoanzia. Inakusaidia kujua kama unakimbia kuelekea mbele au unatelezea nyuma.
Uvumilivu
Kuna wengine wanapoanza tu mambo yananyooka na kuona mafanikio asubuhi ya Mwaka. Wengine inawagharimu maumivu mpaka waone njia iliyonyooka kuelekea mafanikio. Ukiwa na mawazo dhaifu unaweza pangua maazimio kabla ya Mwaka kuisha.
Kushirikisha watu wengine
Msukumo kutoka kwa jamii inayokuzunguka ni muhimu. Ni rahisi kupata ushauri kwa watu waliokuzunguka kuhusu jambo unalofanya pale ambapo unakuwa uliwahi kuwashirikisha. Ni ngumu kumshirikisha mtu mwingine kwa jambo ambalo unaweza kushindwa. Unachoweza kufanya ni kutafuta mtu wa kuangalia uwajibikaji wako kwa hilo azimio. Ni rahisi kuahirisha jambo kwa nafsi yako mwenyewe ila ni ngumu kukubali kushindwa mbele ya mtu mwingine.
Pangia muda
Umewahi kusema unakosa muda, hakuna anayepata muda. Wote tunatumia muda, tunatumia muda kwa mambo ya muhimu. Unachoweza kufanya ni kupanga muda unaoweza kuuelewa na kuufuata. Jambo linalopangiwa muda hufanyika.
Kitu ni zaidi ya patupu
Kuna muda unakuta umefanya kitu kidogo sana kuliko na vile ulivyotarajia. Tofauti ya kufanya kidogo na kutokufanya ni kubwa sana. Nguvu yako katika kufanya kidogo ni muhimu sana kuliko kutofanya kabisa. Jitihada yeyote kuelekea kwenye malengo yako ni muhimu kuliko isipokuwepo.
Anguka inuka haraka
Haijalishi kuwa umeanguka mara ngapi ila kinachojalisha ni umeinuka mara ngapi baada ya kuanguka. Usigeuze anguko la muda mfupi kuwa sababu ya kuvunjika moyo. Vingine ni kukubaliana na anguko na kunuia upya kuelendelea na njia ya malengo.
Azimio kuazimia usipo azimia kuna mtu ataazimia kwaajili yako na utarazimika kutimiza maazimio hayo
World Inspiration Inc tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya kwa kusema AZIMIA 2017
Mwalimu Mwakajila F. A, Jr
C.E.O
World Inspiration Inc.
```Inspired by God 🇹🇿```

Comments