UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI

Utangulizi Kukomboa muda ni dhana inayogusa watu wengi kwa maana kila mtu atamani siku moja awe mmiliki wa muda wake. Kukomboa muda sio sawa na kutunza muda, kama kuna kitu duniani kisichowezekana kutunzika ni muda pekee. Muda ulioutunza jana huwezi kuutumia leo. Unachoweza kufanya ni kutumia muda wote ulionao kwa kufanya mambo ya kimaendeleo, ndio ya kimaendeleo ikiwemo kulala! eeh namaanisha maendeleo binafsi. Kuna wakati Unaweza kuwa umesongwa na kazi nyingi lakini huzalishi kitu na haina maendeleo, je utakuwa umetumia muda vizuri? Sasa unatofauti gani na mtu aliyelala kwa maana ya kupumzika. Unatumia muda, unatunza muda au unakomboa muda? Katika hayo matatu lenye ubora ni Kukomboa muda. Ndio maana naandika kuhusu Kukomboa muda. Ukombozi ni dhana ya kimapinduzi inayobeba maudhui ya kujitoa kafara yani kujitoa sadaka. Hizi ni mbinu za Ukombozi wa muda, kufanya hivyo utakuwa umejitoa sadaka kwaajili ya maisha yako, wengi wanaotumia mbinu ...