UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI



Utangulizi
Kukomboa muda ni dhana inayogusa watu wengi kwa maana kila mtu atamani siku moja awe mmiliki wa muda wake. Kukomboa muda sio sawa na kutunza muda, kama kuna kitu duniani kisichowezekana kutunzika ni muda pekee. Muda ulioutunza jana huwezi kuutumia leo. Unachoweza kufanya ni kutumia muda wote ulionao kwa kufanya mambo ya kimaendeleo, ndio ya kimaendeleo ikiwemo kulala! eeh namaanisha  maendeleo binafsi. Kuna wakati Unaweza kuwa  umesongwa na kazi nyingi lakini huzalishi kitu na haina maendeleo, je utakuwa umetumia muda vizuri? Sasa unatofauti gani na mtu aliyelala kwa maana ya kupumzika. 

Unatumia muda, unatunza muda au unakomboa muda? Katika hayo matatu lenye ubora ni Kukomboa muda.  Ndio maana naandika kuhusu Kukomboa muda. Ukombozi ni dhana ya kimapinduzi inayobeba maudhui ya kujitoa kafara yani kujitoa sadaka. 

Hizi ni mbinu za Ukombozi wa muda, kufanya hivyo utakuwa umejitoa sadaka kwaajili ya maisha yako, wengi wanaotumia mbinu hizi hawatumii kamsa (alarm), inayoaminiwa na wachache kuwakumbusha kuhusu matukio mbalimbali

Tumia Muda
Siku moja ina massa 24, ni muda gani Unatumia kati ya masaa Hayo? Nadhani jibu ulililonalo ni kuwa Unatumia masaa yote.  Sio kila unalolifanya ni jambo la uzalishaji au maendeleo mengine ni Sawa na kupoteza muda, wakati mwingine kuna watu wanatumia muda wako kama wao. Kutunza muda unakuwa na malengo gani juu ya huo muda. Tenga muda tumia muda wote ulionao hakikisha kuwa hakuna sekunde unayoibakiza au kuacha mtu mwingine atumie muda wako kwa kukupangia kitu cha kufanya. Naupenda msemo unaosema “amka kwa kuazimi lala ukiwa umefanikiwa.

Kuwa mtu wa mipango na mikakati
Mikakati hufuata baada ya mipango. Muda hauwezi kukuacha kama wewe ni mtu wa mipango, ni Kweli kuna tabia ya kupanga na kushindwa kutimiza Malengo. Naamini kuwa mtu aliyewahi kupanga mara yingi akashindwa kutimiza mipango ana nafasi kubwa ya kujifunza kuliko yeye ambaye hajawahi panga. Mipango huitaji mikakati ya kutimia. kila mpango lazima uwe mahususi, wazi, Maalum, unalopimika na wenye muda. Kwahiyo ukiwa mtu wa kuweka mipango kwenye maisha yako ghafla hutahitaji kukumbushwa swala la kukomboa muda itakuwa mara chache.

Weka vipaumbele 
Stephen Covey mwandishi wa kitabu cha 7 Habits of Highly Effective People ameelezea kuhusu kufanya kitu cha kwanza kwanza akiwa anahusianisha na kanuni za kuweza kujitawala na kuendesha maisha yako. Kutokuacha mambo yasiyo muhimu kuziba nafasi ya mambo muhimu. Hapa ndio matumizi ya to do list yalipoanzia na kufanya watu wafanye hadi new year resolution. Kuweka vipaumbele ni Kufanya kitu cha Kwanza kwanza. Kubali kuwa una mambo mengi ya kufanya na huwezi kuyafanya kwa wakati mmoja, inakubidi ujipe nafasi ya kufanya yote kwa wakati tofauti tofauti mpaka ufikie malengo yako. Kufanya yote nusu nusu na Kufanya Moja lililokamilika kipi  in bora zaidi? 

Chagua marafiki kwa makini Sana 
Marafiki wabaya hawaharibu Tabia njema tu Bali wanaharibu mfumo Wa maisha ikiwemo swala la muda. Mpaka mtu aitwe rafiki kwako lazima mtakuwa na mfanano Wa mtindo wa maisha, unafanya nini, unaangalia nini, unasikiliza nini na unaangalia nini wakati gani,yote hayo rafiki yako anamchango nayo. Unakutana na watu wapya kila siku Unawezaje kufanya uchambuzi wa rafiki anayekufaa? Kujitambua nini unataka kutoka kwa mtu mwingine ni muhimu sio lazima aendane na wewe lakini akiwa na uwezo kujaza nafasi iliyopungua kwako. ukibaki na msimamo wako mzuri rafiki mbaya ataondoka.

Fanya kitu sasa.
Wakati mwingine kesho huwa haitatokea kama vile unavyotamani iwe, leo ni siku nzuri ya kufanya kinachowezekana ili kesho jambo lingine lifanyike kwa wepesi zaidi. Namna nzuri ya kukomboa muda ni kufanya jambo la thamani leo. Kesho yako itakushukuru sana kwa kutumia leo vizuri. Mlundikano wa mambo mengi kwenye kesho yako utapelekea kesho yenye majuto ya muda kutokutosha na kushindwa kutimia kwa makusudi uliyonayo.

Changua  mambo muhimu
Hii  inataka kufanana na namba tatu na namba tano. Katika yote unayotaka kufanya Changua yale ya muhimu kwanza ndio ufanye na yasiyo muhimu achana nayo. Kwenye mlolongo wa mambo uyotaka kufanya futa kabisa yale yasiyo muhimu na lenga yaliyo muhimu pekee, hapo muda utakutosha na utapata wasaa wa kupumzisha mwili.

Tunza kumbukumbu
Mtu aliye makini anapaswa kuwa na tabia ya kutunza kumbukumbu ya mambo yake au vitu vyake ili kuepusha muda kupotea kwa kurudia jambo Moja mara nyingi. Tunatakiwa kutunza kumbukumbu ya mafanikio, changamoto, mawazo mapya, maamuzi unayofanya na mengine mengi. Kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako ni muhimu sana. 

Weka ratiba
Ratiba ni jambo zuri kwa kukukumbusha kuhusu mpangilio wa siku, juma, hadi mwaka. Ndio chimbuko la kitu kinaitwa almanac inayotumika maofisi makubwa kwa mwaka kuongoza matukio nje ya shughuli za kila siku. Ratiba siku zote huwa na kipengele cha muda wa kutokea kwa tukio husika. Kila sekunde Mungu aliyokupa inahesabu yake, hivyo unatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilisha muda kuwa ni malighafi ya maisha unayoyataka. 

Fanya kitu sasa
Kesho huwa ina mambo yake , kinachowezekana kufanyika leo kifanyike 
Sio kwasababu kesho utafanya tena bali kwa kunuia kufanikisha leo hii hii. Mara nyingi unaweza fanya kitu ukitegemea kupata fursa ya kurudia tena na tena , mantiki yakutunza muda ni kutoona nafasi ya kurekebisha makosa na kunuia kufanya na kumaliza,  kosa likitokea huwa ni nafasi ya kujifunza. 

Weka malengo juu ya swala la kukomboa muda. 
Huwa nipo kinyume na dhana ya kutunza muda,  unatunza muda ili iweje? Pale unapokuwa na uwezo wa kuutumia muda kiufasaha unakuwa umeukomboa haswa. Weka malengo juu ya mkakati wako wa kukomboa muda,  uwe na sababu ya kukomboa muda wako.  Unatamani kuwa na kampuni yako baada ya miaka miwili anza kutumia muda wako kutafuta taarifa sahihi kuhusu wazo lako. Ukiwa huna kitu cha kufanya huwezi komboa muda wako,  maana muda wako hauna thamani. 

Muda ni jambo la kuaminika
Muda ni utaratibu tuliojiwekea ili kuendesha maisha na huwasilishwa kwa nambari.  Muda hauna mwisho wake ni endelevu tu. Kuna kauli zinasema "usipoteze muda wangu"
 na nyingine inasema "muda ni Mali", mali ni jitihada unazotumia ndani ya muda,  muda ni malighafi tu. Kama una kitu cha kujali ni jitihada zako,  juhudi zako.  Muda ni endelevu na usipokuwa makini unaweza jikuta mtunzaji wa muda usio na manufaa kwako .

Muda hauishi bali nguvu ndio inaisha na jitihada inaweza fifia kadhalika uzalishaji unapungua. Sio muda gani umebaki, Bali ni nguvu kiasi gani uliyonayo kumaliza kazi unayofanya.  Wengi wanadhani wanajari muda sana pale wanapomaliza kazi ndani ya muda,  tatizo sio kumaliza Bali umeweza kutumia jitihada zako zote kuzalisha kitu bora kwenye kazi yako. 

"Acha kuwa mtunza muda kuwa mkombozi wa muda"

"Acha kuokoa muda bila sababu,  tumia muda uukomboe"

Muda ni jambo endelevu katika maisha yetu na tujaribu kufanya mambo ya tofauti ndani ya muda mchache tulionao wa kuishi. Usimruhusu mtu atumie muda wako pasipo kibali chako. Siku zote muda ndio unaoongea kuhusu mfululizo wa matukio kwenye maisha yetu na kutupa nafasi ya kutumia jitihada zetu ili kubadilisha mambo. Miujiza mikubwa hutokea ndani ya muda wako kama ukisimama kama kiongozi wa muda wako. 

"Control your presence to change your future".


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.