MWEZI WA NANE

rethink MWANZO MPYA NA YESU KRISTO Neno mwanzo mpya linaweza kuwa ngumu kulielewa na nini kusudi LA kulifanya kuwa kichwa cha chapisho hili,namba ni mafumbo yaliyoanza tumika miaka mingi sana ulimwenguni. Namba ni viwakilishi vya vitu au mambo flani.Leo tuangazie kona ya biblia na namba pamoja na tafsiri yake, na tujikite kwenye namba inayowakilisha mwezi tulionao Wa nane. Namba nane inamaana kubwa kwa Mungu, mpaka kufanya mwanzo Wa juma uwe ni siku ya nane. Kila kitu katika biblia chenye mwanzo mpya kimefungamanishwa na namba nane. Mwezi Wa nane. Mwezi Wa nane ni mwezi unaosimama badala ya mwanzo, ufufuo, na ukombozi Wa mwanadamu kwa damu ya Yesu. (Kuzaliwa upya) Imenifurahisha kuona kuwa Leo ni jumatatu siku ya kwanza ya juma kwa wengi wetu na ni siku ya kwanza ya mwezi. Ila hii sio sababu halisi ya kuwa mwanzo mpya katika mwezi huu. Biblia inasema nini? Mungu aliokoa watu nane kwa safina kipindi cha gharika ya Nuhu, ili aanzishe uzao mpya ulimwenguni. Kama ilivy...