MWEZI WA NANE
rethink
MWANZO MPYA NA YESU KRISTO
Neno mwanzo mpya linaweza kuwa ngumu kulielewa na nini kusudi LA kulifanya kuwa kichwa cha chapisho hili,namba ni mafumbo yaliyoanza tumika miaka mingi sana ulimwenguni. Namba ni viwakilishi vya vitu au mambo flani.Leo tuangazie kona ya biblia na namba pamoja na tafsiri yake, na tujikite kwenye namba inayowakilisha mwezi tulionao Wa nane.
Namba nane inamaana kubwa kwa Mungu, mpaka kufanya mwanzo Wa juma uwe ni siku ya nane. Kila kitu katika biblia chenye mwanzo mpya kimefungamanishwa na namba nane.
Namba nane inamaana kubwa kwa Mungu, mpaka kufanya mwanzo Wa juma uwe ni siku ya nane. Kila kitu katika biblia chenye mwanzo mpya kimefungamanishwa na namba nane.
Mwezi Wa nane. Mwezi Wa nane ni mwezi unaosimama badala ya mwanzo, ufufuo, na ukombozi Wa mwanadamu kwa damu ya Yesu. (Kuzaliwa upya)
Imenifurahisha kuona kuwa Leo ni jumatatu siku ya kwanza ya juma kwa wengi wetu na ni siku ya kwanza ya mwezi. Ila hii sio sababu halisi ya kuwa mwanzo mpya katika mwezi huu.
Biblia inasema nini?
- Mungu aliokoa watu nane kwa safina kipindi cha gharika ya Nuhu, ili aanzishe uzao mpya ulimwenguni.
- Kama ilivyokuwa wanakondoo kwa agano la kale,Yesu alitwaliwa kuwa mwanakondoo kuchukua dhambi zetu katika siku ya kiebrania iitwayo Nisan 10 ( Yohana 12:28-29)aliangikwa siku ya Nisai 14. Ufufuko wake ukatokea,kama vile alivyosema siku tatu baada ya kuzikwa,ambayo ilikuwa mwisho Wa juma sabato ys siku ya Nisan 17. Nisan ilikuwa pia ni siku ya nane tangu Yesu alipopewa hukumu ya msalaba.Yote hata yanadhihirisha ukamilifu Wa Yesu na ushindi wake dhidi ya mauti.
- Watoto Wa kiume walitahiriwa siku ya nane kuonesha kutahiriwa kwa mioyo ya mawadamu kwa ondoleo LA dhambi warumi 2:28-29 WAKOLOSAI 2:11-13
- Siku ya pentekoste siku ya 50 yani baada ya majuma saba tangu ufufuo Wa Kristo Yesu, siku hiyo ni siku ya nane ya juma la saba. Siku hii inasimama badala ya udhihirisho Wa ufufuo Wa mwanadamu kutoka mauti na kupewa mwili mpya 1 korintho 15:20 pia ni siku kuu kama ilivyoainishwa kwenye kutoka 20:4-6.
- Yesu alionekana Mara nane kabla hajapaa kwenda mbinguni
- i)Mariam Magdalena Marko 16:9-11
- ii)Emmau Luke 24
- iii)Kwa wanafunzi wote isipokuwa Tomaso Yohana 20:19-24.
- iv)Kwa wanafunzi wote pamoja na Tomaso Yohana 20:26-29
- v)Kwa watu zaidi ya 500 1 korintho 15:4-7
- vi)Galilaya mathayo 28:16-17
- vii)Galilaya Yohana 21: 1-24
- viii)Kabla ya kupaa kwenda mbinguni matendo ya mitume 1
Kwa miaka mitano sasa Mungu amenionekania katika kipindi kama hiki cha mwezi Wa nane, na nimekuwa nikiona mambo mapya katika maisha ya wengi wanaoamini neno. Kitu cha muhimu ni kulijua neno la Mungu mafunuo kama haya yanafuata baada ya neno. Binafsi tangu nimepata mafunuo haya nimejikita kujua neno zaidi ili nionje wema Wa bwana aliyenikomboa.
Kama bado hujamwamini Yesu kuwa bwana na mwokozi Wa maisha yako, Fanya uamuzi huo sasa unapomaliza kusoma chapisho hili ili ujihakikishie usalama Wa maisha yako mikononi mwake yeye(Yesu) aliyeshinda kifo na mauti….Amen
Mwezi Wa nane ni mwezi wako Wa kubarikiwa na Wa kuanza mwanzo mpya katika kila eneo LA LA maisha yako….Amen
Imeandikwa na :- Mtumwa bila faida
Mwakajila Frank
C.E.O
World inspiration Inc.
Comments