RAMANI YA KUTIMIA KWA MAONO YA MAFANIKIO

HamasikaLeo Maono ya mafanikio ni zaidi ya kuongezeka kiuchumi, kuwa na cheo na kuwa na shahada. Kupanga juu ya mafanikio kunahusisha nyanja zote za maisha. Kama ilivyo kwa ramani, unatakiwa kutambua mambo yafuatayo;- Mwanzo wa safari Mwisho wa safari Usafiri Mkoba wa kusafiria (Hazina ya safari) Mwelekeo/Njia na kiongoza njia MWANZO WA SAFARI. ( Wewe ni nani kwa sasa) Ramani ina mahali pa kuanzia. Mahali pako pa kuanzia ni kujibu swali hili kuwa wewe ni nani kwa wakati huu?. Jibu lako litakuelezea hali yako ya sasa kwamba ni mtu wa aina gani; ni wanafunzi, mfanyakazi, mfanyabiashara au mjasiriamali. Kupata muonekano zaidi wa mwanzo wa safari yako ni unatakiwa kuangalia kwa karibu imani yako, thamani yako na misimamo yako mbali na hali yako ya kiuchumi, kitaaluma na kijamii. Vile utavyojiona huwa ni tofauti na vile ulivyo. " Naitwa Peter, 19, ni mhitimu wa high school" Maneno ya Peter yanatuelezea juu ya ha...