RAMANI YA KUTIMIA KWA MAONO YA MAFANIKIO

HamasikaLeo



Maono ya mafanikio ni zaidi ya kuongezeka kiuchumi, kuwa na cheo na kuwa na shahada. Kupanga juu  ya mafanikio kunahusisha nyanja zote za maisha. Kama ilivyo kwa ramani, unatakiwa kutambua mambo yafuatayo;-
Mwanzo wa safari
Mwisho wa safari
Usafiri
Mkoba wa kusafiria (Hazina  ya safari)
Mwelekeo/Njia na kiongoza njia


MWANZO WA SAFARI.
( Wewe ni nani kwa sasa)

Ramani  ina  mahali pa kuanzia. Mahali pako  pa kuanzia ni kujibu swali hili kuwa wewe ni nani  kwa wakati huu?. Jibu lako litakuelezea hali  yako ya sasa kwamba ni mtu  wa aina  gani; ni wanafunzi, mfanyakazi, mfanyabiashara au mjasiriamali. Kupata muonekano zaidi wa mwanzo wa safari yako ni unatakiwa kuangalia kwa karibu imani yako, thamani yako na misimamo yako mbali na hali yako ya kiuchumi, kitaaluma na kijamii. Vile utavyojiona huwa ni tofauti na vile ulivyo.


"Naitwa Peter, 19, ni mhitimu wa high school"

Maneno ya Peter yanatuelezea juu ya hali  yake kwa sasa, japokuwa hatujafahamu kuhusu imani yake, thamani yake na misimamo yake. Vitu hivyi  ndio vinaweza kumtoa  Peter hapo alipo na kuendelea mbele na safari.

Zaidi unaweza kuangalia kwa makini juu ya madhaifu yako, uwezo wako pamoja na mambo unayopendelea na usiyo pendelea  kufanya. Tabia, hali  na matukio usiyo penda kuyaona kutokea kwako au kwa jamii inayokuzunguka.

Peter alijitambua kuwa ni mtu anayeweza kujipa  motisha binafsi( self motivated), mkarimu, mtoa huduma, ila alikuwa sio mvumilivu. Alipendelea kufanya kazi ya udaktari wa binadamu. Zaidi aliamini kuwa uhai upo ili kutimia  kwa makusudi na vita inaharibu thamani ya mtu.

MWISHO WA SAFARI
(Unataka kuwa nani)

Maono ya vile unataka kuwa. Sababu ya watu wengi kusema kuwa wanataka  kuwa wao huja  pale mtu  anapokuwa na picha ya vile anavyojiona alivyo tangu mwanzo. Niliwahi kuandika chapisho kuhusu namna ya kuwa wewe.

Inayo husiana: Namna ya kuwa wewe


Inatakiwa kujitambua vizuri ili ujue ni nani  unataka kuwa na kufahamu mambo unayotakiwa kubadilika; tabia, mitazamo  na namna unavyoyaona maisha. Kama unapata shida kujitambua mwenyewe ulivyo hivyo ndivyo maono yako na malengo yako yanavyokuwa magumu kutafsiri.

Mwisho wa safari yako unatakiwa kujumuisha kila jambo linalohusu uwepo wako duniani: kimwili, kihisia, kiakili na kiroho.

Kuendelea na hadithi ya peter, baada ya kutambua imani yake, thamani yake na vitu anavyovipa kipaumbele pamoja na misimamo yake katika maisha, alifanya maamuzi kwamba anataka maisha ya kujitoa kusaidia na kuhudumia watu wengine

USAFIRI


Usafiri ni namna unavyoweza kufika mwisho wa safari yako kutoka pale ulipo. Inaweza kuwa wito wa maisha, shughuli unayotakiwa kufanya kufika pale unapopaona kwenye ufahamu wako. Kwa ujumla mikakati ya maisha yako inategemea sana nini unajua juu  yako wewe. Huo wito  wako haukufanyi ufike tu bali, utakapo fika hatua  fulani  wito  unaongezeka na kwenda kwa mtiririko huo mpaka maono yako yatimie jambo ambalo  linachukua sehemu yote ya maisha yako, na ndio maana inaitwa wito wa maisha.

Peter aliamua kuwa anafaa kuwa daktari kulingana na alivyojitambua kwenye hatua zilizopita........
Kuelezea maono na wito wa maisha yake inaweza kuwa hivi: Kuishi maisha ya kujitoa kuhudumia watu wengine kama daktari katika maeneo yanayoathiriwa na machafuko na vita.

MKOBA WA KUSAFIRIA
( Maarifa, ujuzi na mtazamo)

Chakula, vinywaji na dawa  pamoja na mahitaji ya lazima ya safari huwekwa kwenye mkoba. Tumia hili wazo kwenye ramani yako ya maisha, unavyosafiri kukimbizana na maono yako pia unatakiwa kubeba maarifa, ujuzi na namna unavyoyaona mambo yaani mtazamo. Hii hubainisha uwezo wako na kukusaidia kifikia maono yako.



Kuna umuhimu wa kutathmini ni taarifa gani, ujuzi gani na mtazamo gani unao na na unatakiwa kuongeza nini ukiwa safarini. Hii tathmini itakupa muonekano wa mafanikio yako kutoka mbali.

Peter alitambua kuwa anatakiwa kupata maarifa na ujuzi wa kitaalamu kuhusu utabibu ili aweze kuwa daktari. Alitambua kuwa sio mvumilivu juu ya tabia mbalimbali za watu , hivyo hii ndio tabia aliyotakiwa kubadilisha. 

KIONGOZA NJIA NA MWELEKEO

Kiongoza njia kuna kuthibitisha kuwa upo kwenye mkondo sahihi au unafuata ramani, wakati mwelekeo unahusianisha muda wa kusafiri. Mtu akikueleza kuhusu njia ya kufika mahali mara nyingi anakupa na muda kuwa utafika muda fulani. Katika kupanga maisha yako lazima uwe na kiongoza njia na mwelekeo. Kiongoza njia ni kipimo cha mafanikio yako. Kufika Dar es Salaam unapita njia inayoelekea huko na njiani kuna alama za barabara pamoja na vibao vilivyoandikwa majina ya mahali. Kufika chalinze kunakupa ishara ya kuwa umekaribia kufika unapokwenda na wakati mwingine kunakibao kimeandikwa kufika Dar ni Kms kadhaa. Hivyo huwezi kuweka malengo ya kufika Dar kutokea mbeya ndani ya masaa mawili kwa njia ya basi ni jambo ambalo halipo.

Hivyo haiwezekani kuweka malengo ya kuwa na masters pamoja na doctorate degree ndani ya miaka miwili, kwasababu muda wa masters degree pekee ndio miaka miwili.



Turudi kwenye mfano wa peter, aliweka viongoza njia vifuatavyo kwenye ramani yake ya mafanikio: kumaliza shahada akiwa na miaka 25; kubobea kwenye magonjwa ya kuambukiza akiwa na miaka 27; kufanya kazi kwenye hospital ya umma kwa miaka 3 na baadae kuhamia mahali pa machafuko ya vita.

TATHMINI
Umuhimu wa kuwa na ramani ya maisha ni kuepusha mambo yafuatayo:-

  1. Kupotea na kuingia njia isiyo yako na kusafiri  safari ya mtu  mwingine
  2. Kuepusha haraka isiyo na lazima wakati hujui unapokwenda
  3. Kuepusha kupoteza muda pasipo na sababu ya msingi.


Ramani hiyo huweza  kuboreshwa pindi uwapo njiani kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wako. Ndio maana ni muhimu kuweza kukisia kona, matuta, mawimbi na upepo mkali ikiwemo na hali  ya hewa ya mahali unapo safiria.



Siku unazaliwa haikuwa kitu cha kujulikana kwa watu ulimwenguni  kwa sababu hukuwa na kitu wala hukufanya kitu, siku unakufa itakuwa ni siku ya huzuni ulimwenguni kote  kwa kupoteza mtu. Mfano wa watu mashuhuri wengi kipindi walizaliwa haikujulikana lakini leo wakifa sote tunaguswa kuwapoteza, kwasababu wamefanya mambo makubwa  kutokana ndoto zao  kubwa.


Imani yangu ninaendelea  kuujenga ufahamu wako na kukupa mwanzo wa kufikiri upya ili upate mambo mapya kila iitwapo leo.

Na:-
Mwalimu; Mwakajila F.A Jr ðŸ‡¹ðŸ‡¿
C.E.O
World Inspiration Inc
Inspired by God.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI