NAMNA YA KUKABILIANA NA MAWAZO YATOKANAYO NA HOFU.
HamasikaLeo
Habari za uzima ndugu msomaji wangu. Bado tuna endelea na harakati zetu za kujifunza namna ya kutumia uwezo wetu wote tulionao kufanya mambo duniani. Leo tujikite kwenye swala zima la mawazo na hofu katika mchakamchaka wa kufukuzana na maendeleo ya mtu kuanzia kwenye mawazo ya kila siku.
Ni kanuni ya maisha ya kila binadamu kuwaza, shida inakuja pale mawazo yako yanapotawaliwa na hofu, na wakati mwingine kushindwa kutofautisha wazo linalotokana na hofu au Lisilo la hofu. Wengi tunaamua kuishi tu maisha yaendelee.
Kama muda wote unawaza kiasi gani maisha yalivyo magumu kwako, muda wote utahisi kuwa wewe mi maskini kuliko wote.
Hofu ya maisha na kujiona hujafanikiwa hakupelekei mambo mazuri kukujia. Kama unataka kubadilisha maisha yako, badili namna unavyofikiri....na vile unavyosema kwa sauti mbele ya watu. Je, unayowaza na kusema yanatokana na nini?
Ni muhimu kufahamu kuwa haijarishi ni kiasi gani tatizo lako ni kubwa, ni kwa kiwango gani tatizo limekuzidi uwezo, ni mara zote mawazo yatokanayo na hofu na maneno hasi tunayoongea. Kuna wakati unafika tunashindwa kuzuia hayo yote na tunaishi kwenye mawazo ya hofu tukitegemea matokeo yatokanayo na hofu.
Hivyo njia Pekee ya kurejesha mamlaka yako juu ya maisha yako ni kuacha kulalamikia na kuhofia hatma yako, na kuanza kuizungumzisha hiyo sauti kwenye ufahamu wako. Sauti inayokukumbusha kuwa hauwezi, inayokukumbusha namna gani mambo yalivyo magumu.
Mdomo mkubwa ndani ya ufahamu wako ni mfululizo wa mawazo yatokanayo na hofu, hisia za kujikinga na mambo hasi yanayotokea kwenye maisha yako na uzoefu ulionao juu ya maisha.
Kwanini yanatokea?
Kwanini sipati pumziko?
Siwezi kuhimili haya.
Maana yake nini? Hakuna anaejali.
Hayo maswali yanatokea kwenye ufahamu wa mtu anayekufahamu vizuri na unamwamini sana, mtu huyo ni wewe. Unaposhindwa kutunza siri na huyo mtu unajikuta utasema hayo mawazo yako yanayotokana na hofu.
Kujitambua ni hatua ya kwanza ya kushupazia shingo sauti unayosikia kutoka ndani ya ufahamu wako na kuepuka mawazo hasi. Utapo gundua mabaya yatakayo tokea utaacha mara moja. Unaweza ondokana na mawazo yanayotokana na hofu kwa kuwaza, kusoma na kutafuta namna yeyote itakayo kupa fursa ya tumaini, imani, ujasiri, Ushujaa na Uamuzi mpya.
Kitu chochote kinachokushusha chini tambua uwepo wa hofu na Mara moja fanya kuzungumza na hiyo hofu kwa maneno yanayotokana na hisia zako na kwa imani. Wakati mwingine watu huongea maneno yakasikika usijue wanaongea na Nani, ni kujibizana na mtu huyo anayerudisha nyuma maisha ya wengi.
Sikiliza, Hofu. Najua hupo na kitu gani unajaribu kufanya. Lakini hakita wezekana. Haitawezekana kwasababu nimejipanga Kushinda. Nina uamuzi juu ya mawazo gani yatawale ufahamu wangu!
Nina uchaguzi wa maneno yanayotakiwa kutoka kinywani mwangu. Lakini hofu, kuna nguvu kubwa ndani yangu ambayo ni kubwa kuliko chochote utakacho nipiga nacho. Hivyo endelea kushindana na mimi. Kitu kimoja najua: nitashinda.
Unaona ni kiasi gani maneno yenye nguvu kama haya yanaweza kukuinua kutoka kwenye hali yako ya hofu na kukupeleka mbele? Inaleta maana sana pale mtu unapokuwa na mawazo na maneno chanya, unazidi kujihisi jasiri na inakuwa rahisi kuhamisha mitazamo na kuona njia mbadala za kutatua tatizo unalopitia. Kamwe hofu haijawahi kuwa msingi wa kupata mawazo mazuri ya kutatua tatizo.
Ghafla huwezi kuacha kuwaza mawazo hasi, badili mawazo hasi kwa mawazo chanya utakuwa umefika mahali sahihi.
Na:-
Mwalimu Mwakajila F.A Jr
C.E.O
World Inspiration Inc.
Inspired by God of 🇹🇿.

Comments