LATE MWALIMU NYERERE J.K LEGACY

rethink relive

Mwalimu ni kiungo kikubwa cha maendeleo kama akijitambua na kutambulika na jamii husika yenye uhitaji huo. Mwalimu Nyerere alizaliwa Mwaka 1922 April 13 kijijini Butongo, mzanaki huyu hakuwa mzanaki ilipofika wakati wa kupigania Uhuru na ukombozi.
Hi heshima kubwa kushirikishana mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika kupigania Uhuru wa taifa na bara lote la  Africa. Kiongozi ambaye maamuzi yake na hoja zake zilileta matokeo chanya kwa  taifa.

Alisaidia kuundwa kwa TANU Mwaka 1954 kuwa chama cha kisiasa jambo lililo mchukiza gavana wa uingereza Sir.Richard Gordon Turnbull.


Alifanya maamuzi magumu ya kuacha kazi ya ualimu  akiwa Mwalimu Pugu sekondari kama sehemu ya masharti aliyopewa na gavana kuwa achague moja kati ya siasa  au kazi.

Alishikiria maslahi ya wengi kuliko yake...
"Niliogopa. Nikamuuliza Julius ikiwa ninachokisikia ni kweli, alipojibu ndio nikaogopa zaidi. Nikamwambia anachokifanya ni kibaya, Mungu amempa kazi unataka kuiharibu. Lakini akanijibu anachokifanya kitanufaisha wengi taifa lote" (mama mzazi wa Mwl. Nyerere; 1960).

Viongozi mbalimbali wapigania Uhuru walifanya kituo Tanganyika kwasababu ya utayari wake kusimama kupigania Uhuru wa Africa. Uchu wake wa haki na utayari wake kwa maendeleo ya Africa katika nyanja ya Uhuru na maendeleo.

Aliamini Uhuru wa nchi za kusini mwa bara  la Africa unategemeana, mmoja kati ya waasisi wa umoja wa nchi za kusini mwa Africa ujulikanao kama SADC.

Ni baba wa Taifa mhamasishaji na msukumo mkubwa juu  ya Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961, Dec 9 na muungano wake na Zanzibar 1964, April 26 kuunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Aliyekuwa na dhamira ya dhati ya kuunganisha misimamo na utambulisho wa  makabila zaidi ya 120  kwa lugha ya Kiswahili na muundo wa jamii.

Alihamasisha haki, usawa wa kikatiba kwa watu wa  tabaka  zote, dini zote, hali pamoja na jinsia zote. Alihamasisha ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za maendeleo na siasa  wakati huo na kuwapa nafasi ya Uongozi bibi titi ni mfano mzuri.

Uhuru wa Tanganyika Mwaka 1961 ulikuwa msukumo na hamasa kubwa kwa makoloni mengine ya Africa yaliyoamini Uhuru kupatikana bila mtutu na Nyerere alifanya jitihada bila kuchoka kuungamkono malengo hayo kwa Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) Seychelles (1976). Tanzania walitoa msaada wa kisiasa, vitendea kazi na eneo la kukimbilia mpaka uhuru na utawala mabavu ukaondolewa Mwaka 1975 (Mozambique, Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990 (Namibia) na mwisho, 1994 (South Africa).

 Nyerere alisimamia mawazo ya ukombozi, demokrasia na utu katika bara lote la Africa. Pamoja na viongozi wengine wa Africa waliokuwa na mataifa huru mwaka 1963, walianzisha umoja wa nchi za Africa (O.A.U) ambao baadae ulijulikana kama (A.U). Lengo kuu likiwa ukombozi wa bara zima la Africa.

Mwaka 1967, alianzisha siasa ya ujamaa Tanzania kupitia azimio la arusha, siasa ya ujamaa ilitawala Sera zake nyingi tangu hapo.

 Sera zake za ujamaa zilizopelekea kudidimia uchumi, kuongezeka kwa bei za bidhaa na kuibuka kwa ubadhirifu wa fedha kwa wakati huo. Yote haya yalipelekea taifa kutegemea misaada kutoka nje. Mwalimu akakabidhi nchi kwa mrithi wake Alhaji Ali Hassan Mwinyi ikiwa kwenye hali mbaya ya kiuchumi. Haya hayatoshi kumvua sifa kubwa aliyonayo kama muasisi ya Taifa.

Nukuu zaMwalimu:

Huwezi kuendeleza  watu. Unatakiwa kuwapa fursa ya kujiendeleze.


Elimu sio mbinu ya kukwepa umaskini ni mbinu ya kupambana dhidi ya umaskini.

Uhuru hauwezi kuwa wa kweli kama tukiendelea kutegemea zawadi.

Tanzania makabila zaidi 120 yalipoteza Uhuru wao  lakini ni taifa moja tu lililopata Uhuru.

Kwa machache haya napenda  kumalizia kuwa Mwalimu atabaki kuwa baba wa taifa na hamasa kwa vijana kufanya mambo ya tofauti kwa taifa kama alivyofanya Mwalimu kwa mfano..

Imeandikwa na;-
Mwl;- Mwakajila Frank A. Jr
C.E.O
World Inspiration Inc.
Inspired by God for 🇹🇿

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI