TEMBEA MBELE
Nilipokuwa
nafikiria kuhusu mwezi wa tatu tulioanza leo nikakumbuka kitu kuhusu maana
inayofanana na jina la mwezi huu. Mwezi wa tatu kwa kalenda ya Gregorian
tunayotumia unaitwa kwa jina March, lenye maana yake kutokana na asili yake.
Sikutaka kung’ang’ana na maana yake na asili yake ila nikafikiri kuhusu maana
yake kwa lugha ya kimombo. March maana yake ni MWENDO. Tumetembea sana kwaajili
ya mwenge, maadhimisho na mambo mengine mengi kama ishara ya kutiana hamasa.
Mara
nyingi kwenye matukio ya pamoja yanayogusa maisha ya kila mmoja watu huwa
wanaandaa matembezi ya pamoja juu ya swala fulani. Lugha nyepesi wanaita
maandamano ya amani, wengine wanasema matembezi kwaajili ya.......... kuna
sababu kubwa moja ya msingi inayowafanya watu wafanya matembezi.
Watu
hufanya matembezi ili kujenga ufahamu kwa watu wote wanao kerwa na jambo
hilohilo kuwa hawakopeke yao, ndio maana maandamano hayo hayana mwaliko. Mtu
yeyote anaweza kuungana na kundi la watembezi kufanya wanachofanya kama amenia
kuungana bila kuleta vurugu.
Matembezi
ya kupinga ukeketaji, matembezi ya kupinga vifo vya albino, utoaji mimba, siku
ya kisukari na mambo mengine mengi amabyo kila binadamu anaweza kuguswa nayo.
Dhima
yangu sio kukukumbusha ufanya matembezi ya amani, bali ni kukujuza kuwa mwezi
huu ni mwezi wako wa KUSONGA MBELE, kwa yote uliyokuwa umepanga kufanya kwa
mwaka huu na nina uhakika kuwa umeanza kujiweka sawa tangu mwezi wa kwanza.
Hivyo hatua ya pekee kwa mwezi huu ni
kusonga mbele tu.
Ufunuo 22:1-2
Kisha
malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima maangavu kama kioo yakitoka kwenye
kiti cha enzi cha Mungu na Mwanakondoo Mto huo
ulitiririka kupitia katikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huo
kulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumi na mbili kwa mwaka, yaani
kila mwezi; na majani yake ni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa.
Usiwe
sababu ya kutokupata matunda kwenye uliyoyapanga kwa kusitasita kusonga mbele
kwa ushindi. Ukiwa unawaangalia wafanya kazi wanaokuwa wanafanya matembezi ya
mei mosi wakiimba solidarity
forever sio kwamba hawana shida ni kujitia morali wa kusonga mbele.
Ukitaka kuongeza mwendo wa mambo yako unayofanya lazima uimbe wimbo mmoja
kwenye maisha yako yaani uwe na kauli moja ya kufanya jambo sio kuwa kigeugeu.
March up
March
for your life
Frank Mwakajila
Mwandishi
Comments