Posts

MASOMO 23 MWAKA 2017 UMENIFUNZA

Image
HamasikaLeo           Kama hauna ubunifu kila siku, upo  kwenye njia ya kurudi ulipotoka Tabia ya kuahirisha ni mbinu ya kukwepa kufanya vitu vipya. Usifanye kitu kama hakikupi furaha. Kama haujali sana basi haujakua sawasa. Kutokuwa na utulivu Wa mawazo ni ishara ya ukuaji. Kuwa mkarimu, mwenye matumaini, mwema na jasiri katika kila fursa ya maisha. Simu yako inakugharimu kesho yako. Wakati hakuna anayeamini maono yako unatakiwa kuwa mwaminifu kwa maono uliyonayo. Wakati mwingine kitu pekee chenye tija unachoweza kufanya ni kupumzika. Kazinia kusonga mbele badala ya kuwania ukamilifu. Jifunze kwa angalau saa moja kwa Siku, kufanya hivyo kutakufanya uone fursa ambazo wengi hawaoni na utashinda. Kufuta maneno dhaifu kama "siwezi" "haiwezekani" "ni ngumu" na kutumia maneno kama " hii ni nzuri" na " ngoja tujaribu". Kama ukimuhamasisha mtu mmoja kwa siku siku yako haijapotea. Kuishi kwenye historia yako ni kutoheshimu ke...

TISA DISEMBA NA UHURU WA FIKRA

Image
" Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa   fikra " moja ya nukuu za Hayati Mwalimu Nyerere JK. Akimaanisha umaskini unaotokana na fikra za kitumwa, kushindwa au kutopewa fursa ya maamuzi juu ya hatma yako, kuwepo duniani kwa lengo la  kuongeza idadi ya raia  na si  huru  kama wengine. "Hakuna anayeweza kukutawala bila kuanzia kwenye ufahamu wako" utawala mzuri na makini unaanzia kwenye fahamu yani kukufanya utengeneze fikra ya kuwa mtumwa na uwe  umeridhika na kutumika. Siku  hizi neno zuri ni  Mtumishi( ina  maana sawa na mtumwa wakati mwingine lina maanisha mfuasi). Uhuru una maana halisi ya kuwa na haki ya maamuzi binafsi bila ya kuingiliwa na mtu  au taifa lingine. Huwezi kufanya maamuzi yako bila kuhusisha fikra. Kwa maana hiyo mwenye Uhuru Wa fikra pekee ndio raia  huru  kweli na si  vinginevyo. " Mtumwa hata akipewa haki ya kuamua atafanya kama anavyofikiri Bwana wake." Uhuru tuliona...

UNAWAZO GANI?

Image
Mwanzo wa kila kilichowahi kufanikiwa ni wazo, wazo lililobadilishwa na kuwa kitu halisi. Kabla hujawa na wazo hilo unatakiwa kuwa na picha ya wapi unataka kufika au nini unataka kufanya. Inakuwa bahati kama unapata mtu wa kukusaidia kuona picha yako kubwa kuhusu maisha yako, vinginevyo unatakiwa uone mwenyewe hiyo picha na utengeneze wazo la kukufikisha huko. Katika ulimwengu huu tunaoishi mawazo yatakayosaidia makundi makubwa ya watu ndio yanayoweza kushinda na kuishi kwa Muda mrefu.  Wengi wanaoanzisha mawazo huanzia kutoka kiwango cha chini na kuwa na mipango ya kupanda kuelekea juu hadi mawazo yanapowapeleka. Lakini kikwazo kikubwa kwa hili ni kwamba wengi wanaoanzia chini wanashindwa kuinua vichwa kuona FURSA zilizowazunguka kutokana na mawazo waliyonayo kwahiyo wanabaki na mawazo mazuri wakiwa chini. Inatakiwa kukumbuka kuwa mwonekano wa huko chini sio mzuri na unatabia ya kuua tamaa ya mambo makubwa unayoyaona. Wazo hutambuliwa kama chanzo cha utajiri, ...

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

Image
Kamusi sanifu inatoa maana ya thamani kuwa ni hali ya kuwa na faida, manufaa, kitu au mtu mwenye adili. Mtu yeyote anapenda kuwa wa thamani, mtu au kitu kuwa wa thamani inategemea sana matumizi yake na tabia yake, hasa tabia. Tabia ya kitu au mtu ndio hupelekea ubora wake kubaki kama ulivyo au kupungua. Hali na mazingira yanapobadilika kitu bora hubaki kama kilivyo na thanmani yake kuzidi kuongezeka. Chumvi ikichanganywa na mchanga utatafuta mbinu ya kuitoka kwenye mchanga ili uitumie, na ukiamua kwenda kuiuza chumvi hivyo iliyotolewa kwenye mchanga gharama yake haitakuwa ile ya mwanzo. Inaweza kuleta shida kidogo kujadili thamani ya mwanamke pekee wakati huo huo wote wawili mwanamke na mwanaume wanathamani sawa. Nafahamu kuwa wanaume wenzangu wanathamani sawa na mwanamke lakini ukiangalia leo duniani mwanamke huenda hajithamini au athaminiwi jamii yake. Chanzo kikubwa ni mwanamke yeye mwenyewe na ufahamu wake uliojaa mtazamo wa kusaidiwa na kutaka kuthaminiwa pasipo s...

TEMBEA MBELE

Image
Nilipokuwa nafikiria kuhusu mwezi wa tatu tulioanza leo nikakumbuka kitu kuhusu maana inayofanana na jina la mwezi huu. Mwezi wa tatu kwa kalenda ya Gregorian tunayotumia unaitwa kwa jina March, lenye maana yake kutokana na asili yake. Sikutaka kung’ang’ana na maana yake na asili yake ila nikafikiri kuhusu maana yake kwa lugha ya kimombo. March maana yake ni MWENDO. Tumetembea sana kwaajili ya mwenge, maadhimisho na mambo mengine mengi kama ishara ya kutiana hamasa. Mara nyingi kwenye matukio ya pamoja yanayogusa maisha ya kila mmoja watu huwa wanaandaa matembezi ya pamoja juu ya swala fulani. Lugha nyepesi wanaita maandamano ya amani, wengine wanasema matembezi kwaajili ya.......... kuna sababu kubwa moja ya msingi inayowafanya watu wafanya matembezi. Watu hufanya matembezi ili kujenga ufahamu kwa watu wote wanao kerwa na jambo hilohilo kuwa hawakopeke yao, ndio maana maandamano hayo hayana mwaliko. Mtu yeyote anaweza kuungana na kundi la watembezi kufanya wanachofa...

FUNGUO 5 ZA MAAMUZI

Image
                 Kila mtu ni mfanya maamuzi. Tunategemea taarifa na mbinu za kutuwezesha kufanya hayo maamuzi na hapo ndio maamuzi yanapotofautiana baina yetu. Tunapokwenda mgahawani, orodha ya chakula ndio inayotupa nafasi ya kufanya maamuzi kwa kutupa taarifa sahihi za chakula kilichopo mahali hapo. Orodha hiyo ya chakula inafika mbali kwa kutupa gharama ya kila chakula tukakacho kula, hivyo kuweza kupima gharama ya matumizi yetu kabla ya kutumia. Kufanya jambo lolote ia kunahitaji kufanya maamuzi, kwenye biashara, kazi hadi siasa inahitaji maamuzi ya awali. Uamuzi unafanyika katika hali ya kutokuwa na uhakika, wakati ujao haujulikani na wakati mwingine wakati uliopita hali yake ni ya makisio tu. Chapisho hili linaweza kukusadia kukupa mbinu za kukusaidia kuhimiza uwezo wako wa kufanya maamuzi katika ulimwengu tulionao ambao mambo mengi hayanauhakika, hubadilika badilika na wakati mwingine hali nyingine zinazoweza jitokeza zisiz...

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI

Image
Utangulizi Kukomboa muda ni dhana inayogusa watu wengi kwa maana kila mtu atamani siku moja awe mmiliki wa muda wake. Kukomboa muda sio sawa na kutunza muda, kama kuna kitu duniani kisichowezekana kutunzika ni muda pekee. Muda ulioutunza jana huwezi kuutumia leo. Unachoweza kufanya ni kutumia muda wote ulionao kwa kufanya mambo ya kimaendeleo, ndio ya kimaendeleo ikiwemo kulala! eeh namaanisha  maendeleo binafsi. Kuna wakati Unaweza kuwa  umesongwa na kazi nyingi lakini huzalishi kitu na haina maendeleo, je utakuwa umetumia muda vizuri? Sasa unatofauti gani na mtu aliyelala kwa maana ya kupumzika.  Unatumia muda, unatunza muda au unakomboa muda? Katika hayo matatu lenye ubora ni Kukomboa muda.  Ndio maana naandika kuhusu Kukomboa muda. Ukombozi ni dhana ya kimapinduzi inayobeba maudhui ya kujitoa kafara yani kujitoa sadaka.  Hizi ni mbinu za Ukombozi wa muda, kufanya hivyo utakuwa umejitoa sadaka kwaajili ya maisha yako, wengi wanaotumia mbinu ...