DO ONE THING TODAY.....
DO ONE THING TODAY.......
(Review of “The One Thing”)
MATOKEO
YATOFAUTI KATIKA MAISHA YAKO YANATOKEA PALE UNAPOFANYA TOFAUTI.
Mafanikio yanataka umoja wa malengo
yaani kuwa na lengo moja kwa Muda Fulani na kuliwekea mikakati ya kutimia.Unatakiwa
kufanya mambo machache kwa matokeo mazuri, na sio mambo mengi yenye matokeo
mabovu.
Doing same things over and over and
exepecting different result….
Uchu
wako katika kufanya jambo hupelekea mgawanyo wa muda mwingi katika jambo hilo.
Hivyo hupelekea matokeo mazuri yatayofanya ufurahie kazi hiyo na kuifanya zaidi
na zaidi. Na uchu zaidi na muda zaidi
utawekeza katika kazi hiyo au jambo hilo. Inakuwa mzunguko wa matukio katika
maisha.
Watu
wengi wanaopoangalia nyuma kwenye safari ya maisha yao mara nyingi mambo
hawakuyafanya ndio yanayo wavunja mioyo. Wala yale waliyoyafanya hayawafanyi
kujipa moyo sababu ni madogo sana.
Hakikisha
kwenye maisha yako unafanya yale yanayofaha haswa yani yenye tija kuliko.
Utakapo tambua yale yanayofaa haswa kila kitu kitakwenda sawa, usipotambua yale
yanayofaa kitu chochote utaona sawa kukifanya.
Maisha
makamilifu yanapimwa kwa njia nyingi njia moja wapo ni kuishi bila lawama au
majuto.
KUFANYA
MAMBO MAWILI KWA WAKATI MMOJA NI SAWA NA KUTOKUFANYA
Kanuni ya kufanya jambo ni
muunganiko wa kufanya kwa uwezo wako wote pia kufanya jambo hilo vile
linavyotakiwa kufanywa.Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni uwongo, mtu huyo
huyo ni mchungaji, mwigizaji,mtangazaji wa luninga na redio, mshauri na
sahaa,mhamasishaji na bado ni baba wa familia. Kuna mambo mengi atayafanya vile
yasivyotakiwa, mara nyingi inakuwa hivyo katika harakati za kutafuta riziki.
Siku ina sekunde 86400 mwanzo
niliona chache sana, tangu nilipotambua lengo la kuwa ndani ya muda huo
ninaamini hizi ni sekunde nyingi sana kufanya mabadiliko katika maisha yangu. Sio
kwamba tuna muda mchache wa kufanya mambo yetu ila ni kwamba tunajisikia
kufanya mengi sana katika wakati tulio nao. Siamini kwamba lengo la maisha ni
kuwa na furaha, bali ni kutumika, kuwajibika na kujitoa.
Matokeo
mazuri na yasiyo ya kawaida, hutokea pale unapojitoa kwa vyote ulivyonavyo, ili
kuwa vile unavyotakiwa kuwa. Napenda kusema mara nyingi na wanafunzi wangu
nikifundisha“ if you can’t risk the usual, be ready to settle for the ordinary”.
My quote:-
“People
who are crazy enough to think they can change the world are the only one who
do.”
Mwl:
Frank Mwakajila
C.E.O
World
Inspiration Inc
“Inspired
by God living to the limits of our potentials”
Comments