SOKOINE LEGACY

SOKOINE LEGACY
(Father of villages development in Tanzania)

Edward Moringe Sokoine aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa  Tanzania Mara mbili. 1977-1981 ikiwa awamu ya kwanza, 1983-1984 awamu ya pili ambayo hakuimaliza. aliyeiongoza katika kipindi kigumu sana cha kiuchumi na kuwa mwiba mkali kwa wahujumu uchumi.

Sifa za kiongozi

  • Kujiamini
  • Kuheshimu nafsi yako 
  • Kuheshimu mambo ya mwanzo ili kuendelea mbele
  • Aliye na njaa asipewe uongozi




Sokoine dhidi ya wahujumu uchumi na wazembe

Misimamo yake inatupatia taswira ya Tanzania tunayoitamani. Swala la kodi na wafanyakazi hewa ni yaleyale yaliyopigiwa kelele Zama hizo kwa jina la wahujumu uchumi na wabadhirifu.


Hizi ni baadhi ya nukuu za kauli za Sokoine:-


“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - 26 Machi 1983


“Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?” - 23 Oktoba 1983

“Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” - 4 Oktoba 1983


“Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha” - 24 Septemba 1983

“Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri” - 23 Oktoba 1982


“Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi” - 1Februari 1977.

Tanzania ikiwa ni nchi inayojikongoja kukimbia umaskini, ikiwa ni ya 25 kwa nchi maskini duniani huku central Africa ikishikiria nafasi ya juu kwa umaskini. Tunahitaji kiongozi mwenye nguvu ya kuthubutu.

Najivunia kuishi Zama za Tanzania ya Nyerere na Sokoine katika kipindi kupitia makaratasi.

Kipindi hiki ni Kipindi chenye mfumo tofauti wa kiuchumi yaani ubepari, soko huria, uwekezaji, mapinduzi ya viwanda, ubinafsishaji, na mengine mengi yanayoletwa na utandawazi uliokithiri.

Mfumko mkubwa wa sayansi na teknolojia inayotulemea na kushindwa kuitumia ipasavyo. Nadhani imekuja kwa kuwahi.

Sera za kijamaa zilizoboreshwa kutumika katika kipindi cha ubepari na kuandikwa kwenye makaratasi zinazosuasua kutumika.

Mzawa akitamani kushikiria uchumi wa taifa anaishia kuwa na tamanio, tunajivunia fursa nyingi tulizonazo lakini hazitufaidishi.

Vijana ndio tunu ya taifa na uhusishwaji wao kwenye michakato ya kiuchumi ndio tija pekee tuliyonayo.

Tukikosa viongozi wenye weledi wa kuongoza tutakimbia mbio zisizo na manufaa

Siasa imevamiwa na watu wenye njaa wasio weza kujizuia kukomba chakula kwenye sahani ya umma.

Turejee Tanzania ya ujamaa ndio tunaweza kujua Tanzania ipi tunahitaji. Sikurudishi kwenye ujamaa ila nataka ufikirie maendeleo ya Tanzania sio yako pekee kwa kuwa kwa kipindi hiki cha Magufuli hutaweza kudumu.

Imeandaliwa na:-
Mwl. Mwakajila✍🏿
C.E.O
World Inpiration Inc.
"Inspired by God; living to the the limits of our potentials.
sky is the limit".

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE WA THAMANI NA TABIA ZAKE 30

KUJIKATAA.KUKATALIWA.KUKATA TAMAA.

UNAWEZAJE KUKOMBOA WAKATI